Meneja wa Manchester United, Ruben Amorim, alipoulizwa kwa nini hamchezeshi Marcus Rashford, alijibu: "Sababu za kutomchezesha mshambuliaji huyo ni zile zile — haoneshi ari wakati wa mazoezi pamoja na mtindo wake wa maisha ya kila siku.
Kama mambo hayatabadilika, nami sitabadilika. Hali ni sawa kwa kila mchezaji; ukijitahidi na kufanya mambo sahihi, tunaweza kukupa nafasi katika kikosi.
"Amorim aliendelea kusema: "Unaweza kuona kwamba tunakosa mchezaji mwenye kasi kwenye benchi, lakini bora kumchezesha kocha wa makipa, Jorge Vital, uwanjani badala ya kumtumia mchezaji ambaye hajitolei kwa uwezo wake wote."
Kwa sasa, Rashford hajacheza mechi za Manchester United kwa wiki sita, huku kukiwa na tetesi kwamba anaweza kuondoka kwa mkopo kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa mwishoni mwa wiki hii.