Kwa mara ya kwanza Pep Guardiola ashindwa kushinda hata mechi moja baada ya mechi 6 mfululizo.  /Picha: Getty

Manchester City imetoka sare ya mabao 3-3 na Feyenoord ya Uholanzi kwenye Uwanja wa Etihad katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League). Hii ni baada ya kuongoza kwa mabao 3 kabla ya wapinzani kusawazisha.

Kwa mara ya kwanza, Manchester City imeshindwa kushinda hata mechi moja baada ya kucheza mechi sita chini ya uongozi wa Pep Guardiola.

Haya yanajiri baada ya Pep Guardiola kuongeza mkataba wake kama kocha wa Manchester City kwa misimu miwili zaidi, siku ya Alhamisi tarehe 21 Novemba, 2024.

Arsenal yaicharaza Sporting Lisbon kwa mabao 5 -1. /Picha: Arsenal

Wakati huo huo, Arsenal ilipata ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno kwenye Uwanja wa Estádio José Alvalade.

Nayo Bayern Munich ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Barcelona nayo iliondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brest, huku Inter Milan ikiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya RB Leipzig.

TRT Afrika