Dabi ya mwisho kuchezwa Goodison Park yamalizika kwa vurugu

Dabi ya mwisho kuchezwa Goodison Park yamalizika kwa vurugu

Liverpool inaongoza katika Ligi Kuu ya England ikiwa na pointi 57.
Hii ilikuwa mechi ya mwisho ya dabi kwa Everton katika uwanja wa Goodison Park, wanatarajiwa kuhamia uwanja wao mpya wa Bramley-Moore Dock. /Picha: Soccertonic

Dabi ya mwisho ya Merseyside katika Uwanja wa Goodison Park ilimalizika kwa sare ya 2-2 kati ya Everton na Liverpool.Everton walitangulia kwa bao la Beto kabla ya Alexis Mac Allister kuisawazishia Liverpool.

Mohamed Salah aliipa Liverpool uongozi, lakini James Tarkowski akafunga goli la kusawazisha dakika ya 98 ya mchezo.

Baada ya mechi, vurugu zilitokea, na kusababisha wachezaji na makocha kadhaa, akiwemo Arne Slot wa Liverpool, kupewa kadi nyekundu.

Hii ilikuwa mechi ya mwisho kwa Everton kuwa wenyeji wa Liverpool katika uwanja wa Goodison Park, kwani wanatarajiwa kuhamia uwanja wao mpya wa Bramley-Moore Dock mwanzoni mwa msimu wa 2025-2026.

Kwa upande wa Liverpool, sare hii bado imewahakikishia uongozi Liverpool kwenye Ligi Kuu ya England wakiwa na pointi 57, wakifuatiwa na Arsenal wenye alama 50. Everton wako nafasi ya 15 wakiwa na pointi 27.

TRT Afrika