Biden Solar Energy / Photo: AP

Ufungaji huu wa umeme wa photovoltaic utajengwa katika eneo la hekta saba, kilomita 200 kutoka Lubumbashi.

"Tuna takriban paneli 4368 za wati 550 ambazo zitawekwa kwenye eneo la hekta saba. Mradi huu mkubwa utatoa nishati ya umeme kwa maelfu ya kaya katika sehemu ya Kusini-Mashariki mwa DRC. Ni mradi wa wakongo wenyewe kwa asilimia mia," alisema. Eric Monga, mkurugenzi wa kampuni ya Kipay Investment.

Wakazi wengi wa eneo hilo la nchi wamefurahi na wanatamani mradi huu ukamilike haraka iwezekanavyo ili kufidia kukatika kwa umeme.

Katika maeneo mengi ya nchi, wafanyabiashara wa samaki kama Aline Kasongo wamekosa umeme kwa zaidi ya wiki moja na wanatumia jenereta ili kutunza samaki wake wasiharibike.

“Nasubiri siku ya uzinduzi niunganishwe na njia hizi za umeme kwa sababu kila mara nimekuwa nikitupa samaki wengi ambao huharibika kwa kukosa umeme na hivyo kuleta hasara kubwa ya fedha,” analalamika Aline Kasongo, mfanyabiashara anayeuza samaki katika soko la Lubumbashi.

"Mradi huu ni msaada kwetu. Serikali ya Kongo iwape vifaa vyote kampuni hii ili uwekaji umeme wa jua ukamilike kwa wakati" anaongeza Bw. Kasongo.

Ujenzi wa mtambo huu wa umeme wa photovoltaic ni wa kwanza katika eneo hili na utatoa megawati 2.4 za umeme na unaweza kukamilika mwisho wa mwaka 2024, kwa gharama ya jumla ya dola milioni 600 za uwekezaji.

DRC ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na zaidi ya maeneo 780 yaliyoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme mdogo na mkubwa, yenye uwezo wa megawati 100,000.

TRT Afrika