Umeme Uganda umerudi baada ya kukatika kote nchini kwa masaa kadhaa

Umeme Uganda umerudi baada ya kukatika kote nchini kwa masaa kadhaa

Umeme umerudi katika baadhi ya maeneo, Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Uganda (UETCL) ilisema.
Mtazamo wa jumla unaonyesha mji mkuu wa Kampala nchini Uganda / Picha: Reuters

Uganda ilikumbwa na kukatika kwa umeme kote nchini kwa saa kadhaa Ijumaa, kampuni yake ya umeme ilisema, ikiongeza kuwa umeme ulikuwa ukirejeshwa taratibu jioni ya leo.

Kukatika kwa umeme kulifanyika wakati wa majaribio ya kituo kipya cha kuzalisha umeme wa maji chenye uwezo wa megawati 600 kilichojengwa na Wachina kwa gharama ya dola bilioni 1.5 kwenye mto Nile kaskazini mwa nchi hiyo, Kampuni ya kuzalisha Umeme Uganda Limited (UETCL) ilisema katika ukurasa wao wa mtandao wa X.

"Kampuni ya Ugavi wa Umeme ya Uganda Limited inafahamisha umma kuwa kukatika kwa umeme kitaifa kumeripotiwa kufuatia jaribio la kukataa mzigo katika kituo cha umeme cha maji cha Karuma," kampuni hiyo iliandika kwenye X Ijumaa.

Katika post lingine masaa mawili baadaye, ilisema umeme ulikuwa umerudi katika baadhi ya sehemu.

Uganda ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,000, kulingana na wizara ya nishati.

Inazalisha umeme zaidi ya inavyotumia na imekuwa ikichunguza uwezekano wa kuuza ziada hiyo kwa majirani kama Sudan Kusini na Kenya.

Reuters