| Swahili
Simu za mkononi zinazouza vizuri zaidi duniani
Hapa kuna orodha ya simu janja zilizouza vizuri zaidi duniani kihistoria tangu kuanzishwa kwa matumizi ya "smartphone"
Simu za mkononi zinazouza vizuri zaidi duniani
simu za mikononi zimekuwa katika maisha yetu ya kila siku bila kujali | Picha: Getty  i / Others
8 Februari 2024

Kulingana na utafiti wa kampuni ya utafiti wa teknolojia ya International Data Corporation(IDC) bidhaa za Transsion (Tecno, Itel, na Infinix) zilitawala mauzo ya simu janja barani Afrika kuelekea mwisho wa mwaka 2023, huku bara la Afrika likichangia zaidi kwa kuingiza Transsion katika orodha ya wauzaji 5 bora duniani kwa mara ya kwanza kabisa Samsung ilishika nafasi ya pili barani wakati Xiaomi ikawa ya tatu.

Hata hivyo ukiacha Samsung, hakuna kampuni nyingine iliyofikia mauzo mengi ya jumla ya simu janja, angalau kwa sasa.

Ndani ya miongo minne, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika miundo na maumbo ya vifaa hivi, kutoka miche ya sabuni, matofali hadi kuwa na mionekano ya kuvutia kwa watumaiji wa vifaa hivyo vya mawasiliano.

Lakini ni dhahiri kwamba matoleo ya kwanza ya simu yalifanya vizuri sokoni na yanaendelea kufanya hivyo mpaka leo.

Ifuatayo ni orodha ya simu janja zilizofanya vizuri zaidi katika mauzo kihistoria.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp Channels

CHANZO:TRT Afrika