Kampuni hio kubwa ya teknolojia inalenga watumiaji wa mitandao kutoka nchi na maeneo mapya.
Lugha zingine zinazozungumzwa sana zilizojumuishwa katika juhudi za upanuzi ni Kichina, Kijerumani, Kihispania, Kiarabu na Kihindi, huku kampuni ya kimataifa ikisema kuwa kipengele cha uandishi kinatumika kwa hadi lugha nane sasa.
Bard ni huduma ya mazungumzo ya AI ya Google inayofanya kazi kwa karibu na ile ya ChatGPT, na tofauti pekee ni kwamba Bard inatoa habari kutoka tovuti mbalimbali.
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, limeorodhesha Kiswahili kati ya lugha 10 zinazozungumzwa sana ulimwenguni kote na zaidi ya wazungumzaji milioni 200, na kuashiria thamani inayowezekana ambayo Bard itapata kutokana na upanuzi huo.
Google ilisema katika taarifa: "Bard inatafuta kuchanganya upana wa maarifa ya ulimwengu, akili na ubunifu wa miundo mikubwa ya lugha ya Google. Inatumia taarifa kutoka mtandaoni ili kutoa majibu. Kama teknolojia ya majaribio, mara kwa mara Bard inaweza kutoa taarifa zisizo sahihi kujibu maswali ya mtumiaji."