Vyombo vikubwa vya kutengeneza filamu na vipindi vyta televisheni Hollywood vilitangaza kuwa kufikia Agosti mosi watakatisha mikataba yao na waigizaji filamu na waandishi iwapo hakutapatikana muafaka juu ya mgomo wanaofanya.
Shirika la Reuters liliripoti kuwa limepata vidokezo kutoka kwa jarida la Variety lenye 'sikio ndani ya Hollywood.'
Kuanzia Mei 2, muungano wa waandishi wa filamu wa Hollywood, Writers Guild, walitangaza mgomo wao ambao uliungwa mkono mara moja na wasanii wengi wa Hollywood.
Mgomo huo unaaminiwa kudumaza shughuli za uzalishaji filamu na vipindi vya televisheni - matokeo yake ikiwa kufungwa kwa series zinazoendelea au kusitishwa kutolewa fimau zozote mpya.
Taarifa iliyochapishwa na jarida la Forbes Marekani inakisia kuwa mgomo huu unasababisha hasara ya dola 150 Milioni kwa siku.
‘’Athari za kifedha ni kubwa na zinaweza kuongezeka mara dufu.’’ Anasema Andrew Boyd, mshauri wa jarida la kifedha la Finty. ‘’Iwapo mgomo huo utaendelea hadi 2024 au zaidi, inaweza kuleta madhara kubwa zaidi.’’
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, mgomo huu unakisiwa kuleta hasara ya takriban dola Bilioni tatu huku baadhi wakikisia hata hasara ya zaidi ya dola bilioni nne.
‘’Gharama hii inajumuisha ucheleweshaji wa uzalishaji, kuongezeka kwa matumizi mara tu mgomo utakapotatuliwa na uwezekano wa kushuka kwa ubora wa uzalishaji wa filamu.’’ Anasema Andrew Boyd.
Vuta nikuvute ni kwa sababu gani?
Waandishi wa filamu ndio walioanza mwezi Mei wakidai nyongeza ya mishahara na marupurupu ikiwemo kuendelea kupokea marupurupu ya mauzo inayopatikana baada ya filamu zao kuchapishwa.
Mgomo huu uliungwa mkono na wadau wengi katika tasnia hiyo ya filamu huku muungano wa waigizaji unaowakilisha zaidi ya waigizaji 160 000, nao ukitangaza kujiunga nao.
Kufikia Julai 13, Waigizaji walitanagaza nao mgomo wao. Miongoni mwa mambo waliyokuwa wakidai ni kuongezewa mishahara, marupurupu kwa filamu zinazouzwa nje ya Marekani na hakikisho kuwa hawatapokonywa kazi zao na kupewa kwa Akili Bandia, AI.
Kila baada ya miaka mitatu kampuni kubwa za kuzalisha filamu husaini mikataba mipya na waigizaji na waandishi wa filamu. Ilipofikia Mei 2023 na mikataba hii ikawa imechelewa kutengenezwa, wadai hao waliingia katika mgomo.
Mfumo wa kutazama filmau moja kwa moja yaani ‘Streaming’ ilibadilisha namna waandishi wa filamu wanalipwa na hasa wakati wa COVID.
Sasa waandishi hao wanataka mikataba mipya iweze kufunika hilo pia.
Kila mara filamu zinaporudiwa, matangazo ya biashara inaendelea pia, na kiasi fulani cha pesa hizo zinalipwa kwa waandishi.
Lakini hii imevurugwa na kuwa mitandao ya kutazama filamu kama vile Netflix na Prime pamoja na nyinginezo ambazo zinahifadhi filamu nyingi na series za televisheni kuweza kutazamwa na wateja wao wakati wowote wapendao. Hii imeondoa fedha za matangazo ya biashara.
Wanaoathriika na mgomo huu
Filamu na vipindi vya televisheni vinavyotengenezwa nchini Marekani ndivyo vinaathirika na mgomo.
Filamu ambazo zilikuwa hazijakamilishwa kutengenezwa zimekomea hapoa pamoja na seriea kama vile Greys anatomy, SNL na The Daily Show na nyinginezo pia zimesitishwa.
Kwa filamu ambazo zilikuwa tayari kutolewa zinaathiriwa na kuwa wasanii waigizaji hawajitokezi kuzizungumzia katika vyombo vya habari na kukutana namashabiki kwa hiyo mauzo yanaanguka.
Hata hivyo vipindi vinavyotoka nje ya Marekani vitaendelea, kwa hiyo iwapo wewe ni mpenzi wa filamu za Korea au Bollywood au Nollywood na nyingine pia nje ya Marekani, utaendela kupokea vitu vyako.
Pia vipindi vya habari, na Reality Show zitaendelea bila wasiwasi.