Hali ya biashara ni ngumu sana haswa kwa biashara ndogo ndogo barani Afrika, zinazotaka kujiinua. Biashara hizi zimekuwa misingi kwa makampuni mengi ya sekta binafsi kote barani Afrika na kwa hakika, sehemu kubwa ya dunia.
Wawekezaji hawa wanatoa zaidi ya asilimia 80 ya ajira barani Afrika na ni wachangiaji muhimu katika pato la taifa la nchi wanazofanya kazi.
Kwa hivyo, sio siri kwamba upanuzi wa sekta binafsi kupitia upanuzi wa biashara ndogo ndogo ni muhimu kwa uundaji wa nafasi za kazi na ukuaji wa uchumi ambao Afrika inahitaji katika miongo michache ijayo.
Ustawi wa Afrika siku za usoni unategemea ukuaji na mafanikio ya biashara za Kiafrika na kupitia kwao uundaji wa njia salama za kujipatia riziki kwa idadi inayoongezeka ya vijana wa bara hilo.
Kuna fursa kubwa kwa biashara barani Afrika kujiendeleza zaidi. Idadi ya zaidi ya watu bilioni 1.2 ni soko tayari, pamoja na mfumo wa umoja wa Afrika wa eneo la biashara huria la barani Afrika likiendelea.
Gharama za uendeshaji biashara ni kubwa kutokana na upungufu wa miundombinu ya kuinuia uwekezaji mdogo, kama vile mitandao ya uchukuzi haitoshi na upatikanaji mdogo wa umeme. Pia kuna uhaba wa wafanyakazi wa usimamizi wenye uzoefu kusaidia kukuza biashara.
Mtaji unahitajika ili kuepukana na changamoto hizi na kufanya uwekezaji kwa ukuaji. Lakini biashara nyingi ndogo zinahitaji fedha zaidi kuliko zinavyoweza kufikia ili kukuza biashara zao na mikopo ya benki inaweza kuwa ghali sana, kwa sababu ya viwango vya juu vya riba.
Suluhisho ya kuziba pengo la kifedha kwa biashara nyingi hizi ni uwekezaji wa kibinafsi, pamoja na wawekezaji wa kibinafsi, fedha za mitaji, taasisi za fedha za maendeleo, usawa wa kibinafsi na kupitia mipango ya ubia.
Kuongezeka kwa teknolojia pia kumefungua fursa mpya za kupokea mtaji kupitia ufadhili wa watu wengi na makampuni kama vile ‘Auspicious Blockchain’ inayounganisha wawekezaji binafsi wanaoishi nje ya bara na biashara ndogo ndogo barani.
Changamoto ni nini?
Mara nyingi, kuna "pengo la kisheria" kati ya wawekezaji kwa upande mmoja na wafanyabiashara wadogo wa Kiafrika kwa upande mwingine. Kupitia kazi yetu hapa kampuni ya Strand Sahara, tumetambua changamoto kadhaa za kisheria ambazo biashara ndogo ndogo za Kiafrika hukabiliana nazo.
Hazithaminiwi!
Biashara chache sana ziko na uwezo wa kufaulu majaribio yanayohitajika ili kufikia uwekezaji wa kibinafsi, haswa kwa sababu ya utunzaji duni wa kisheria na kifedha na kushindwa kupitisha miundo ya kisheria ya biashara. Kushindwa huku kunapunguza thamani ya biashara, kwani wawekezaji au wakopeshaji watarajiwa hawatakuwa na hakikisho wanalohitaji kuwa uwekezaji wao katika biashara utakuwa mwafaka.
Hazina habari
Wamiliki wa biashara ndogo ndogo mara nyingi hawajui mahitaji ya usimamizi wa shirika, kama vile kuchagua muundo sahihi wa kisheria wa biashara na kuingia katika makubaliano yanayofaa na wanahisa, wakurugenzi na wafanyakazi wakuu. Hii pia inahusu ulinzi mwingine wa kisheria wa biashara, kama vile wa kutosha mikataba ya biashara, mikataba ya ajira na ulinzi wa haki miliki.
Hii inazuia uwezekano wa uwekezaji na pia ni sababu kuu ya kushindwa kwa biashara kudumu kwa muda mrefu.
Hazihudumiwi
Huduma za kisheria za kibiashara mara nyingi zinazohitajiwa na wamiliki wa biashara ndogo ndogo huwa ngumu kupata.
Wanalalamika kwamba inachukua muda mrefu sana kupata majibu wanayohitaji au kutatua shida yao, na inabidi waendelee kukazana kujimudu na changamoto zao. Mara nyingi hawana uhakika ni pesa kiasi gani itawagharimu kutatua changamoto zao kabisa, na kwa kawaida ni zaidi ya ilivyotarajiwa.
Suluhisho
Hakuna shaka kwamba biashara ndogo ndogo zinahitaji huduma za kisheria za kibiashara ili kuwasaidia kupata fedha na kujitayarisha kwa ukuaji. Kuna haja ya wanasheria kuelimisha wamiliki wa biashara ndogo umuhimu wa huduma hizi za kisheria.
Wanasheria wanapaswa kuzingatia kuunda bidhaa na huduma iliyolenga kusaidia biashara ndogo kuelewa mahitaji ya kisheria kabla ya matatizo yoyote kutokea, kuwaonyesha mapungufu yaliyopo, na kisha kutoa bidhaa na huduma wanazohitaji kuziba mapengo hayo. Wanasheria pia lazima watafute njia za kufanya kisheria huduma zinazopatikana kwa urahisi zaidi, uwazi na kwa bei nafuu kwa biashara ndogo ndogo.
Haya ndiyo tunayofanya kupitia mtandao wetu wa http://www.strandsahara.com.
Mwandishi, Rashida Abdulai, ni mwanasheria aliyeshinda tuzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Strand Sahara, mtoa huduma za kisheria mtandaoni kwa biashara