Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limepanga kuanza safari za moja kwa moja kuelekea Johannesburg, Novemba 30, 2024./Picha: Air Tanzania

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limepanga kuanzsisha tena safari za moja kwa moja kuelekea Jonannesburg nchini Afrika Kusini.

Kulingana na ATCL, safari hizo ambazo zitakuwa mara tano kwa wiki, zinatarajiwa kuanza Novemba 30, 2024.

Ratiba iliyotolewa na ATCL kwenye ukurasa wake wa X, inaonesha kuwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kuelekea Johannesburg kuanzia siku ya Jumatatu, Jumatano, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kila wiki.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa ATCL kuwa na safari za kuelekea nchini Afrika Kusini.

Wakati ikitambulika kama ATC, shirika hilo lilingia kwenye makubaliano na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) kuwa na safari za namna hiyo, mpango ambao ulidumu kwa kipindi cha miaka 10, kuanzia mwaka 2003.

TRT Afrika