Upenyaji wa mtandao bado uko chini katika sehemu nyingi za Afrika. Picha: kumbukumbu ya AP

Maswali kadhaa yanaweza kujitokeza kupitia kwa majibizano hayo. Moja, ni kwa nini huduma ya setilaiti ndogo sana (VSAT) inayotolewa na Musk imevutia watu wengi ingawa si ya ajabu? Pili, je utoaji wa intaneti kwa satelaiti una thamani gani kibiashara?

Na hatimaye, kwa nini mijadala hiyo inafanyika kwenye mitandao ya kijamii wakati inaweza kukamilishwa kupitia njia zinazofaa kiofisi au mazungumzo hayo yamevuka hatua hio?

Je, kitu gani kiko mezani?

Ifahamike kwamba ni asilimia 26 tu ya wakazi wa Afrika Mashariki wamefikiwa na huduma ya intaneti, kulingana na taariza kutoka Statista za mwaka 2022. Wakazi wa maeneo ya vijijini wana ufikiaji mdogo wa intaneti kuliko wale wa maeneo ya mijini barani Afrika.

Ili kupata huduma ya Starlink, lazima kwanza uzingatie maeneo ambayo teknolojia ya Musk inajaribu kufikia. Upatikanaji wa umeme na gharama kando - je, watu tayari kufunga mitambo yake kulingana na bei ya sasa?

Starlink inatoa kifurushi cha GB 1,000 chenye kasi ya 150Mbps kwa malipo sawa na shilingi 2,357,000 nchini Tanzania, ikiwa kiwango cha juu kuliko watoa huduma wengi nchini. Zaidi ya hayo, wanapanga kutoa huduma za setilaiti kupitia minara wa simu ambazo makampuni ya ndani yatahitaji msaada wa ziada ili waweze kushindana.

Kuna tahadhari, hata hivyo, gharama ya vifaa na ufungaji, japo ni malipo ya mara mmoja, bado vina gharama kubwa na pia vina mapungufu. Kwa mfano, tuseme hali ya hewa ni ya kusuasua. Katika hali hiyo, huduma inasumbua, mfano halisi ni kile kinachotokea wakati wa kutazama chaneli za Multichoice wakati mvua kubwa inanyesha.

"Huduma za Musk sio ya ajabu lakini zina faida ya kuwa nafuu zaidi kwa soko na husambazwa kwa gharama ya chini. Kuna uwekezaji mkubwa nyuma yake ikilinganishwa na washindani ambao wamejaribu kuunganishwa na Afrika kwa mtindo huo." Anafafanua mjasiriamali-mbunifu, Jumanne Mtambalike.

Watoa huduma wa ndani katika eneo hili, kama Safaricom ya Kenya na Tigo ya Tanzania, walianza kusambaza 5G yenye kasi ya hadi 500Mbps; utanukaji bado unahitaji zaidi na mtumiaji anahitaji kifaa maalumu (router).

Watu ambao kawaida hutumia huduma za VSAT ni wamiliki wa nyumba za mapumziko, watafiti maporini na wanausalama wanaofuatilia mienendo ya watu fulani.

Je, kuna sera za aina gani?

Watoa huduma za satellite wanaweza kukusanya mapato kutoka mbali na kuajiri idadi ndogo ya wafanyakazi ili mfumo uendelee kufanya kazi.

Starlink ni mojawapo ya watoa huduma wakuu wa mtandao nchini Tanzania. Picha: Reuters Archive

Kampuni hiyo imeshirikiana na Umoja wa wadau wa Mawasiliano Afrika (ATU) ili kuwezesha uanzishwaji wa Starlink barani Afrika.

ATU ni shirika la Kiafrika linalounganisha nchi na watoa huduma za mawasiliano ya simu ili kuongeza maendeleo ya miundombinu ya teknolojia ya habari na mawasiliano barani humo. Umoja wa Afrika na ATU wameunda mfumo wa udhibiti unaoruhusu kampuni kurusha satelaiti zake na kusambaza mtandao katika nchi zote za Afrika.

Kuna sababu nzuri kwa nchi za Afrika Mashariki kukataa Starlink na kushikamana na watoa huduma wa mawasiliano wa ndani. Ikizingatiwa kuwa wengi wao hutoa ajira kwa walipa kodi wengi, wanafuata sheria za nchi na wanaweza kudhibitiwa kwa matakwa ya mamlaka iliyoko madarakani.

“Inawezekana Serikali bado hazijaikumbatia teknolojia hiyo kwa sababu zimeangalia uwezekano wa kukosekana kwa utulivu katika ushindani sokoni na pia wamebaini kuwa hii inaweza kuua kampuni za simu za ndani ambazo zina idadi kuwa ya watu waliowaajiri na kwa kiasi gani wanachangia pato la nchi." Anaongeza Mtambalike.

“Inawezekana Serikali bado hazijaikumbatia teknolojia hiyo kwa sababu zimeangalia uwezekano wa kukosekana kwa utulivu katika ushindani sokoni na pia wamebaini kuwa hii inaweza kuua kampuni za simu za ndani ambazo zina idadi kuwa ya watu waliowaajiri na kwa kiasi gani wanachangia pato la nchi."

Jumanne Mtambalike, Mjasiriamali Mbunifu

Katika maeneo ya mbali yenye miundombinu mibaya, huduma hio itakuza uchumi wa kidijitali. Hata hivyo, kuna maeneo ambayo gridi ya taifa haiwezi kuhudumia hio teknolojia ya satelaiti. Hii ni changamoto kwa watoa huduma za satelaiti na serikali ya Tanzania. Atayeweza kufikisha huduma huko kwa wananchi ndio atakuwa mshindi wa kupata wateja.

Pale ambapo ukanda fulani unapoazima ukurasa kutoka kwa serikali zilizopita - ikimaanisha kuruhusu teknolojia ya satelaiti kuingia nchini kama mtoa huduma, kuna sababu ya kuamini kuwa kutakuwa na upinzani kwa vile vikwazo fulani vitapunguzwa.

Jumanne Mtambalike fundi teknolojia anahisi Musk ana faida zaidi ya washindani kutokana na uwekezaji wake mkubwa. Picha: Jumanne

Mfano wazi unatokana na chaguzi za hivi majuzi wa mwaka 2021 nchini Uganda na Tanzania mwaka 2020 ambazo mtandao wa ndani ulizimwa wakati wa kipindi cha uchaguzi na kufifisha shughuli fulani na kuwanyamazisha wafichuaji maouvu kadhaa. Kitu ambacho hakingetokea kupitia utoaji wa intaneti ya satelaiti.

Watumiaji wa sasa wa teknolojia hii wanasema nini?

Nigeria ni mojawapo ya nchi za kwanza barani Afrika kukumbatia teknolojia na imekuwa na huduma za Starlink tangu Januari.

"Mnaaijeria wa wastani atakuwa na shida na gharama za ufungaji vifaa maalum, lakini hilo likishafanyika, kuna manufaa kwa makundi makubwa (kama familia) kutumia huduma hiyo tofauti na kampuni za mawasiliano za ndani zinazotoa intaneti kwa ukomo." Kabir Ibrahim ni Mhandisi wa Mtandao kutoka Nigeria.

Tangu kuzinduliwa kwa huduma hio tarehe 22 Februari nchini Rwanda, mtumiaji mkubwa ni Serikali.

"Ni mapema sana kutathmini jinsi matumizi yatakavyokuwa, lakini kwa mtazamo wa mambo, malengo ni vituo vya serikali kama shule za maeneo ya pembezoni, visiwa na maeneo ya mbali vijijini ambapo ni vigumu kuunganisha huduma licha ya upanuzi wa miundombinu ya teknolojia." Anafafanua mwandishi wa habari wa Rwanda Johnson Kanamujire, aliyeangazia uzinduzi wa huduma kwa kampuni hiyo.

Kwa upande mwingine, Kenya itakuwa ikitumia huduma hiyo katika robo ya pili ya mwaka. Kinachofanya huduma za satelaiti kuwa kikwazo kikubwa ni kifaa cha kuanzia cha sawa na shilingi 1,885,600.

Moses Kemibaro, Mchambuzi wa Teknolojia na Vyombo vya Habari vya Dijitali kutoka Nairobi, aliagiza vifaa vyake vya kuanzia kwa lengo la "majaribio", akiangalia kama hii inaweza kuwa mbadala wa kile kinachopatikana kwa sasa.

Kasi ya intaneti inapopungua au kushuka na kupanda inakulazimu urudi kwenye simu yako kwa sababu intaneti ya nyumbani sio ya kutegemewa kila wakati, kwa hivyo kuwa na kifaa cha pili au kununua kipya sio jambo gumu kwangu

Moses Kemibaro, Mchambuzi wa Teknolojia na Vyombo vya Habari vya Dijitali

Ucheleweshaji wa nchi kama Tanzania kwa sasa una mengi nyuma yake. Pamoja na kwamba kuna pesa za kupata kutoka kwa serikali, pia kuna uhuru mwingi unaokuja kutoka kwa watoa huduma kama hao kwenda kwa watumiaji.

Starlink ni mojawapo ya huduma nyingi za setilaiti zinazogonga mlango, lakini angalau bei ni nafuu kidogo. Huku washindani kama Microsoft wakiwa njiani wakiwa na ahadi za kutoa intaneti kwa kwa mataifa yanayoendelea, swali linabaki, je eneo hilo liko tayari kwa utoaji mbadala wa Intaneti?

TRT Afrika