Rais Emmerson Mnangagwa alishinda awamu yake ya pili ya uchaguzi kwa asili mia 52.6% ya kura/ Picha: Others 

Serikali ya Zimbabwe imewaita wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya kwa mkutano katika mji mkuu, Harare, ambapo ilishutumu waangalizi wa uchaguzi wa umoja huo kwa upendeleo katika ripoti yao ya awali kuhusu uchaguzi mkuu uliomalizika hivi punde.

Serikali ilishutumu Ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa EU (EU EOM) kwa "uingiliaji mkubwa" katika masuala ya ndani ya nchi na kupotosha ulimwengu kuhusu uchaguzi wa Zimbabwe.

Rais Emmerson Mnangagwa alishinda awamu yake ya pili ya uchaguzi kwa 52.6% ya kura, lakini upinzani umekataa matokeo kwa madai ya wizi na ukandamizaji wa wapiga kura.

Katika ripoti yake, ujumbe wa waangalizi wa EU ulisema uchaguzi "ulipungukiwa na viwango vingi vya kikanda na kimataifa".

Lakini waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe alisema ripoti hiyo "imejaa upotoshaji na madai", kulingana na taarifa ya Jumatatu.

"Ni vibaya sana kwamba EU EOM ilifanya maoni kulingana na uvumi, na kwa msingi wa taarifa za upande mmoja kutoka kwa upinzani," Amon Murwira. sema.

"Kwa maoni yetu, ujumbe wa waangalizi hauna mamlaka ya kisheria ya kutoa maoni kuhusu katiba na sheria zetu, na kutoa matamko ya hukumu kuhusu uchaguzi wetu," aliongeza.

Ujumbe wa waangalizi wa EU unatarajiwa kutoa ripoti ya mwisho kuhusu uchaguzi na maelezo juu ya matokeo ya uchaguzi.

Uchaguzi huo uliofanyika wiki iliyopita, ulikuwa wa pili tangu kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo Robert Mugabe kuondolewa madarakani mwaka 2027.

TRT Afrika