Mwaka huu huku dunia ikiadhimisha silku ya polio duniani Shirika la Afya Duniani, WHO limesema bara limepiga hatua kubwa kutokomeza ugonjwa huu.
Poliomyelitis (polio) ni ugonjwa wa virusi unaoletwa na virusi vya polio, unaoambukiza na kuathiri watoto chini ya umri wa miaka 5.
Virusi huenezwa na mtu mmoja hadi mwengine hasa kupitia njia ya kinyesi, mdomo au, mara chache zaidi, maji machafu au chakula.
Virusi huongezeka ndani ya mwili na huweza kuvamia mfumo wa mwili (nerve system) na kusababisha kupooza kwa baadhi ya viungo.
"Kutoka visa 438 vya polio zilivyoripotiwa mwisho wa Septemba 2022, kwa sasa tunaona hadi kesi 304 katika kipindi kama hicho mwaka huu. Hii inamaanisha kupungua kwa 31% katika idadi ya kesi katika kipindi cha miezi 12 iliyopita," Mkurugenzi wa WHO Africa, Dkt. Matshidiso Moeti amesema katika taarifa yake.
Nchi 21 katika za Afrika bado zinakabiliwa na milipuko ya polio inayozunguka kwa wakati huu.
Baadhi yao iko katika maeneo ambayo hayapata maambukizi ya polio kwa miongo kadhaa.
"Nchi wanachama zimetangaza kukabiliana na polio na kuchukua hatua nyengine za dharura za kiafya wakati wa milipuko," Dkt. Matshidiso amesema na kuongeza, "Uratibu wa mipaka kwa ajili ya hatua za pamoja za nchi kufuatilia virusi vya polio na chanjo ya watoto katika hatua inayoendelea kuwa kipaumbele kukomesha polio."
Mpaka sasa hakuna tiba ya Polio, lakini kuna chanjo ambazo zinatumika kwa ajili ya kuzuia na kuwalinda watoto maishani mwao.