Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula Duniani, World Food Programme, inasema kuwa Sudan inakumbwa na changamoto ya ongezeko ya idadi ya watu wenye wanakumbwa na njaa.
"Uhaba wa chakula unaosababishwa na migogoro umesababisha watu milioni 20.3 kuwa katika hali ya njaa kali," WFP ilisema ijumaa, " kati ya takwimu hizo, watu milioni 6.3 - asilimia 13 ya wakazi wa Sudan - wanakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa."
Sudan imekuwa katika vita vikali kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha Rapid Support Forces tangu 15 Aprili mwaka huu.
"Tangu katikati ya Aprili, mzozo umeendelea kuenea, na mienendo yake imekuwa ngumu zaidi. Kufiikia watu wanaohitaji msaada wa chakula cha kuokoa maisha yao pia imekuwa changamoto zaidi, " Eddie Rowe, mkurugenzi mkuu wa WFP Sudan amesema.
Changamoto zingine za msaada kufikia wanao na uhitaji ni pamoja na wizi wa chakula na mahitaji mengine ya msaada, maafisa wa mashirika ya kibinadamu kuuawa au kushambuliwa.
Pia mchakato yakupata idhini ya kupitisha msaada, maafisa wa kibinadamu wa kigeni na usafiri wa maofisa wa kibinadamu inachelewa sana.
WFP yapata mafanikio
WFP ilipata mafanikio makubwa wiki iliyopita, na kufanikiwa kupeleka msaada wa chakula katika jimbo la Darfur Magharibi, ambalo limeathiriwa pakubwa na mzozo huo.
Msafara wa malori matano yakisafirisha tani 125 za bidhaa za chakula kutoka mashariki mwa Chad hadi Darfur Magharibi, iliwezesha shirika hili la Umoja wa Mataifa kusafirisha msaada wa chakula wa thamani ya mwezi mmoja kwa watu wapatao 15,400 Rowe alisema.
"Ni matumaini yetu kwamba njia hii kutoka Chad itakuwa njia ya kawaida ya kibinadamu kufikia familia hizi huko Darfur Magharibi, hasa katika Geneina - mji mkuu wa Darfur Magharibi - ambako maisha yamesambaratishwa na ghasia," aliongeza.