Waziri Mkuu wa Uingereza kupinga uamuzi wa mahakama kusimamisha uhamishaji wa wahamiaji kwenda Rwanda

Waziri Mkuu wa Uingereza kupinga uamuzi wa mahakama kusimamisha uhamishaji wa wahamiaji kwenda Rwanda

Mahakama ya rufaa imetoa uamuzi kwamba mpango wa serikali ya Uingereza wa kuwapeleka wakimbizi waomba hifadhi nchini Rwanda ni batili kisheria
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunaka amesema hakubaliani na maamuzi ya mahakama kuwa kuwatuma wahamiaji kwenda Rwanda ni kinyume na sheria / Picha: AFP

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amesema huku anaheshimu mahakama kimsingi hakubaliana na maamuzi yao, na kuwa si halali kuhamisha wahamiaji Rwanda.

"Tutaomba kibali cha kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu katika mahakama kuu," waziri mkuu Sunak amesema katika taarifa.

Serikali ya Uingereza imekuwa ikipanga kuwatuma wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza kwenda Rwanda.

Hii ni sehemu ya mpango wa takribani dola milioni 148 iliyokuwa na nia ya kuwazuia watu kuvuka kuingia Uingereza kutoka Ufaransa na boti ndogo.

Majaji walisema kuwa Rwanda haiwezi kuchukuliwa kuwa nchi ya tatu salama, baada ya mpango huo kukashifiwa vikali na makundi ya kutetea haki za binadamu.

"Ninaamini kwamba serikali ya Rwanda imetoa uhakikisho unaohitajika kuthibitisha kwamba hakuna hatari kwamba wanaotafuta hifadhi kuhamishwa chini ya sera ya Rwanda hawatarejeshwa kimakosa," Sunak ameongezea.

Baada ya maamuzi ya mahakama siku ya ya Ijumaa, Rwanda ilisema kupitia taarifa kuwa bado iko tayari kuhakikisha mpangoilio huo unatimia, ikidai kuwa Rwanda ni nchi salama na inaheshimika na shirika la kutetea wakimbizi la UNHCR.

TRT Afrika