Huduma ya Wanyamapori ya Kenya, Kenya Wildlife Service inasema wamemuokoa pundamilia alieyekuwa amepigwa mshale.
"Timu ya Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS) ikiungwa mkono na Mara North Rangers na Sheldrick Wildlife Trust ilikimbia kumsaidia pundamilia aliyekuwa amepigwa mshale," KWS imesema katika mtandao wa X.
KWS inasema walimtibu na kumshughulikia kupitia upasuaji papo hapo ili kuchomoa mshale.
"Pundamilia huyu alikuwa na bahati, mshale ulikosa viungo vyake muhimu na haukusababisha madhara makubwa," shirika la Sheldrick Wildlife Trust limesema katika mtandao wake wa X.
Sheldrick Wildlife Trust ni shirika linalohusika katika uokoaji wa wanyama kama tembo na kuhifadhi wanyamapori na maeneo yote ya nyika nchini Kenya.
Mshale huo haukuwa umesababisha majeraha makubwa.
Wataalamu hao wanasema mtoto huyo wa pundamilia anatarajiwa kupona kabisa.
Ni muhimu kuzingatia kuwa wanyama wana hatari ya kuwindwa na majangili na wawindaji haramu porini.