Maafisa wa upelelezi Kneya wanafanya msako wa madawa ya kulevya/ Picha kutoka X ya DCI Kenya

Maafisa wa upelelezi nchini Kenya wamepata dawa za kulevya zinazoshukiwa kuwa kokeni, katika msako unaoendelea dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya jijini.

"Katika operesheni iliyoendeshwa huko Buru Buru mapema leo asubuhi, wahudumu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya walivamia nyumba moja na kukuta vidonge 18 vya dawa hiyo," Kitengo cha upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya ilisema kupitia taarifa ya mtandao wake wa X.

Washikiwa wawili walikamatwa

Pia zilizonaswa katika msako huo wa saa kumi na mbili asubuhi ni pesa taslimu za shilingi za Kenya na fedha za kigeni, zinazoaminika kuwa zilitokana na ulanguzi wa dawa za kulevya.

 Katika msako mwingine maafisa wa usalama wamepata watu na zaidi ya dola 92.00 kwa pesa za Kenya/ Picha kutoka X ya DCI Kenya

Pesa hizo zilijumuisha $12,601, Euro 15, Ksh509, 495, Tshs 24,000 na Kwanza ya Angola 10,000.

Uvamizi wa leo unafuatia operesheni ingine Jumanne, iliyopelekea kukamatwa kwa watu wanne , akiwemo mama mmoja anayeaminika kuwa mmoja wa wasambazaji wakubwa wa bangi katika jiji hilo.

"Wakati wa msako huo, zaidi ya dola 92.000 zilipatikana pesa taslimu na shehena ya magunia 26 yaliyojaa bangi ilinaswa," taarifa ya DCI imesema,

TRT Afrika