Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la "Allied Democratic Forces" (ADF), wanaoaminika kuwa na uhusiano na kundi la Daesh, wamewaua takriban watu 10 katika shambulio la usiku katika kijiji kimoja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, afisa wa eneo hilo na kiongozi wa mashirika ya kiraia alisema Jumamosi.
Watu wenye silaha walishambulia kijiji cha Masala katika eneo la Beni, kilicho katika mkoa wa Kivu Kaskazini, usiku wa kuamkia leo, msimamizi wa kijeshi Charles Euta Omeonga aliambia Reuters kwa njia ya simu.
Kiongozi wa mashirika ya kiraia Justin Kavalami alisema shambulio hilo lilitekelezwa na wanachama wa ADF, kundi lile lile ambalo afisa wa eneo hilo alilishutumu kwa kuhusika na shambulio lingine la kijiji ambalo liliua takriban watu 16 mapema wiki hii.
Kavalami alisema zaidi ya watu 13 waliuawa katika shambulio la Masala.
ADF wanatokea nchi jirani ya Uganda. Sasa ikiwa na makao yake mashariki mwa Kongo, imeahidi utiifu wake kwa kundi la Daesh na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara, na kuzidi kuyumbisha eneo ambalo makundi mengi ya wanamgambo yanaendesha harakati zao.
Reuters ilisema haikuwezekana kupatiana kwa maoni ya ADF.