Mwigizaji wa Nigeria Richard Mofe-Damijo alipokea Tuzo ya Mafanikio ya Maisha katika Tuzo za 12 za Africa Movie Academy mnamo 2016. Picha: TRT Afrika

Waigizaji watano wa filamu kutoka Nigeria ni miongoni mwa wanachama 398 wapya wa Oscar Academy, ambao watapiga kura kwa wanaoteuliwa kuwa washindi mwezi Machi 2024.

Watano hawa ni mwigizaji tajika Richard Mofe-Damijo, watayarishaji wa filamu Jadesola Osiberu na Kunle Afolayan, mwandishi wa filamu Shola Dada na mkurugenzi wa filamu CJ Obasi.

Akizungumzia kuongezwa kwake kwenye bodi ya Oscar Academy, Dada alisema kwenye Facebook kuwa anamshukuru sana Mungu kwa heshima na fursa hiyo

Iwapo Wanigeria wote watano watakubali ombi la uanachama, watajiunga na bodi ya Oscars ambayo ina watu 10,817. Nyota wa muziki Taylor Swift ni miongoni mwa washiriki wapya kwenye bodi hiyo.

Sherehe ya 96 ya Tuzo za Oscar Academy itafanyika katika Ukumbi wa michezo wa Dolby huko Los Angeles, Marekani mnamo Machi 10, 2024. Picha: AA

Wanachama hao wapya wameongezwa kuchukua nafasi ya wale waliostaafu, waliofariki au kupandishwa cheo.

Kazi mashuhuri

Oscars ni heshima kwa kazi bora ya filamu inayoamuliwa kila mwaka na Academy of Motion Picture Arts au bodi ya filamu iliyochaguliwa kuamuwa filamu na wasanii bora katika tasnia ya filamu pamoja na wahusika na wafanyakazi.

Oscar Academy kilisema kiliwaruhusu wanachama wapya kwa sababu "wamejipambanua kwa michango yao katika sinema."

"Oscar Academy inajivunia kuwakaribisha wasanii na wataalamu hawa katika uanachama wetu. Wanawakilisha talanta ya ajabu ya kimataifa katika taaluma za sinema na wameleta athari kubwa kwa sanaa na sayansi ya picha za sinema na kwa mashabiki wa sinema ulimwenguni kote," Mkurugenzi Mtendaji wa Oscars Academy Bill Kramer na Rais wa Oscars Academy Janet Yang walisema katika taarifa ya pamoja mnamo Juni 28.

Wanachama hawa watastahili kupiga kura katika toleo la 96 la Tuzo za Oscar, zitakazofanyika Machi 10, 2024, ni 9,375.

Kufuatia nyongeza hizo mpya, uanachama wa Oscar Academy wa 2023 utajumuisha 40% ya wanawake, 34% wakiwa na uwakilishi mdogo wa jamii za kikabila au rangi na 51% wanachama wanaotoka nchi nje ya Marekani.

Bodi ya Oscars | Picha: AFP

Ili mtayarishaji wa filamu, mwongozaji, mwandishi au mwigizaji kupata uteuzi wa Oscar, anahitaji kupata kura kutoka kwa wanachama katika tawi lao la kupiga kura.

Idadi ya kura zinazohitajika itategemea ukubwa wa tawi. Matawi makubwa zaidi ni ya Picha Bora ambazo zinahitaji angalau kura 100.

Mfumo wa uzani

Kampuni ya ukaguzi, PricewaterhouseCoopers (PwC), kisha hutumia mfumo changamano wa kuweka uzani ili kubaini walioteuliwa kwa kila aina.

Baada ya kuwafahamu walioteuliwa, wanachama wote wanaweza kuwapigia kura washindi husika. Baadhi ya vitengo, hata hivyo, vinahitaji wanachama kuona walioteuliwa kabla ya kupiga kura yao.

Picha Bora huamuliwa na wanachama kuorodhesha chaguo zao kulingana na wanavyoona sawa, huku PwC ikijumlisha washiriki waliochaguliwa kama nambari moja na wanachama tofauti.

Ikiwa filamu itapata zaidi ya asilimia hgamsini ya kura, itashinda. Ikiwa haifanyi hivyo, basi filamu yenye alama ya chini kabisa itaondolewa kati ya walioteuliwa. Upigaji kura unaendelea hadi filamu ipite kiwango cha uidhinishaji cha asilimia hamsini(50%).

Kujumuishwa kwa wasanii watano wa sinema wa Nigeria katika bodi ya Oscar Academy ni kiashirio cha maendeleo makubwa ambayo tasnia ya filamu barani Afrika, haswa Nollywood kutoka Nigeria, imefanya katika nyanja ya kimataifa.

TRT Afrika na mashirika ya habari