Wabunge wa Afrika Kusini wapiga kura kufunga ubalozi wa Israel

Wabunge wa Afrika Kusini wapiga kura kufunga ubalozi wa Israel

Bunge la Afrika Kusini limepiga kura kufunga ubalozi wa Israel nchini humo
Wabunge mia mbili arobaini na wanane wa Afrika Kusini walipiga kura ya kuunga mkono kufungwa kwa ubalozi wa Israel nchini humo tarehe 21 Novemba 2023. / Picha: Reuters

Bunge la Afrika Kusini limepiga kura kufunga ubalozi wa Israel nchini humo.

Siku ya Jumanne, wabunge 248 katika Bunge la Taifa walipiga kura ya kuunga mkono kufungwa kwa ubalozi huo, na kusimamishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.

Tisini na moja (91) walikuwa wamepiga kura kupinga kusitishwa kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Afrika Kusini imekuwa ikitoa sauti kubwa kuhusu uungaji mkono wake kwa watu wa Palestina kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel dhidi ya Gaza.

Wapalestina takribani 13,300 wameuawa na mashambulizi ya anga ya Israel tangu Oktoba 7.

TRT Afrika