Jumuiya za SADC na Afrika Mashariki, zimetoa wito wa kusitishwa vita DRC.  / Picha: AFP

Mapigano kati ya waasi wa M23 na vikosi vya Kongo yameaanza tena Jumanne katika eneo la Lubero, jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kundi la waasi la M23 limeshambulia kwa mabomu ngome za jeshi za Kongo katika mji wa Kivisire, baada ya waasi hao kuwaua "raia mmoja na wanajeshi wa Kongo" katika shambulio la bomu Jumapili, kwa mujibu wa shirika la habari la Actualite.cd.

“Sasa (1600GMT) tunasikia milio ya silaha nzito hapa Ndoluma, ambapo tuko kwenye mazishi ya raia aliyeuawa wakati wa shambulio la waasi ambalo limelenga wanajeshi wetu siku ya Jumapili. Milio hayo yanatoka Kivisire,” vyanzo vya ndani viliiambia Actualite.cd.

Mapigano hayo yaliibuka baada ya viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kutaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika mkutano wa pamoja uliofanyika Jumapili.

Waasi wa M23 sasa wanadai udhibiti wa Goma na wametangaza utawala wao wenyewe katika mji huo.

Tangu Januari 26, zaidi ya watu 3,000 wameuawa, 2,880 wamejeruhiwa na zaidi ya 500,000 wamekimbia makazi yao, idadi hio ni pamaoja na watu milioni 6.4 ambao tayari wamekimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kinshasa imeishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na kutuma vikosi vyake mashariki mwa Kongo wakati mashambulizi ya hivi punde yalipoanza. Kigali imekanusha mara kwa mara madai hayo.

AA