Polisi nchini Kenya imeonya wananchi kutoingia katika maeneo yaliyohifadhiwa. Hii inakuja huku wananchi hasa katika mitandao ya kijamii waliopanga kufanya maandamano katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta, mjini Nairobi.
"Tungetaka tuwakumbushe umma kuhusu mipaka ya kisheria inayotawala upatikanaji wa maeneo yaliyohifadhiwa, Sheria ya Maeneo ya Hifadhi ... ya kenya inazuia uingiaji wa watu waasioidhinishwa katika maeneo ambayo yametangazwa maeneo ya hifadhi," taarifa ya polisi imeonya.
Waandamanaji wamedai kuwa wanataka kuingia eneo la JKIA kupinga madai ya uwanja huo kuuziwa nchi ya kigeni.
"Amri ya maeneo yaliyohifadhiwa kama ilivyofafanuliwa chini ya Sheria yake. Ratiba ya pili ni pamoja na LPG kiwanda cha lami, bohari za mafuta zilizo katika kituo cha usafiri wa anga cha Embakasi JKIA ," Polisi imesema.
Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Kenya Ports Authority, imetoa tahadhari kwa wasafi kufika katika uwanja wa ndege mapema.
Nayo kampuni ya ndege ya taifa ya Kenya, Kenya Airways ilitoa taarifa kuwaomba wasafiri kufika katika uwanja wa ndege angalau saa nne kabla ya wakati wa safari yao.