Serikali ya Kenya imehimiza wazazi kupeleka watoto wao shuleni huku baadhi ya walimu wakianza mgomo wao katika sehemu tofauti nchini.
“Baada ya mazungumzo kati ya Tume ya Utumishi wa Walimu na vyama vya wafanyakazi, Serikali kwa mfano, imetoa rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja wa mwaka 2021-2025, kuanzia tarehe 1 Julai, 2024," Waziri wa Elimu Julius Migos amesema.
"Serikali pia imetoa rasilimali za kuandaa upya walimu kwa ajili ya utekelezaji wa Mtaala unaozingatia Umahiri,” Migos alisema.
Chama cha Kitaifa cha Walimu Kenya (KNUT), ambacho kiliunga mkono mgomo huo awali ,kimebadilisha msimamo na kuomba wanachama wake kurudi kazini.
KNUT Jumapili iliwaambia wanachama kuripoti shuleni kwani muungano huo umeanza "kushughulikia masuala yaliyosalia."
Ilisema uamuzi wake ulitokana na serilkali kukubali kuwapandisha vyeo asilimia 39 ya walimu 130,000 ambao wamekwama katika nyadhifa zao kwa muongo mmoja.
Tume tayari imewapandisha daraja walimu 51,232 kupitia usaili wa ushindani, huku mchakato ukiendelea kikamilifu,” alisema.
Zaidi ya hayo, alibainisha kuwa makato ya wahusika wengine, ambayo yalikuwa yanasubiri, yametumwa katika benki za biashara, vikundi vya fedha vyaa walimu, miradi ya uwekezaji na majukumu mengine ya kisheria. Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) ilithibitisha kuwa walimu wataendelea kupata huduma katika hospitali za umma na za kibinafsi.
Lakini chama kingine kimekataa, na kusema kitaendelea na mgomo.
Muungano wa Walimu wa Elimu ya Baada ya Elimu ya Msingi (KUPPET) bado umesisitiza washiriki wao kutojihusisha na taasisi za masomo kwa kile wanachodai kushindwa na Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja ya 2021/25 (CBA).
Katika mkutano wa Baraza la Uongozi la Kitaifa la KUPPET Jumapili, wanachama 68 wa Muungano huo walipiga kura kuunga mkono mgomo huo.
Walimu wanataka serikali itekeleze Mkataba wa Makubaliano ya Pamoja wa 2021/25 (CBA).
CBA zilitiwa saini mnamo Juni 2021 na kurekebishwa na nyongeza mnamo Agosti 2023 ili kuwapa walimu mapato bora.
Awamu ya kwanza ilipaswa kutekelezwa ifikapo Juni 30, 2024, na awamu ya pili ilianza Julai 1, 2024.
Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa TSC Nancy Macharia alisema kufuatia majadiliano hayo, serikali ilitoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa awamu ya 2 ya CBA kuanzia Julai 1, 2024.
Walimu wengine wanaendelea na mgomo wakidai kuwa wanataka serikali itimize makubaliano yao ya mapato ya juu na kupandishwa vyeo kwa walimu zaidi.