Freeman Mbowe aliachiliwa mwendo wa saa tano usiku kutoka kituo cha Oyster Bay, jijini Daresalaam/ Picha: X- Chadema 

Mwenyekiti wa chama cha upinzani Tanzania CHADEMA, FreemanMbowe ameachiliwa kwa dhamana kutoka kituo cha Oyster Bay jijini Daresalaam alikokuwa anashikiliwa tangu Jumatatu Mchana.

Mbowe pamoja na viongozi wengine wa chama na wafuasi waliachiliwa kwa dhamana bila masharti.

''Bado sijawaona viongozi wenangu ambao walikuwa wameshikiliwa katika vituo mbali mbali tofauti vya polisi. Hadi Kesho tutakapo pata taarifa kamili juu yahali zao, wako wapi, ndipo tutakapofanya utaraltibu wa kuongea na vyombpo vya habari,;; alisema Mbowe muda mfupi baada ya kuachiliwa kituoni.

Mbowe aliwaelezea waandishi wa habari kuwa wamekata akutoa maelezo yoyote kwa polisi hadi watakapofika mbele ya mahakimu, kwa kukosa imani na wasimamizi wa vituo hivyo.

Alipohojiwa iwapo ataendelea na maandamano, Mbowe alikataa kujibu akisema kuwa atatoa maelezo baadaye.

''Msiulize kama bado tutaendelea kuandamana lakini mtambue wakati wote kwamba maandamano ni haki y akikatiba,'' aliongeza Mbowe.

Viongozi hao wamefunguliwa mashtaka kuwa waliandamana bila kibali, ambapo polisi wamesisitiz akuwa walikataa kutoa kibali kutokana na dalili kuwa maandamano hayo 'yalikuwa na nia ya kuleta uvunjifu wa sheria'.

wengine walioachiliwa kwa dhamana ni Naibu Mwenyekiti bara Tundu Lissu, pamoja na Naibu Katibu Mkuu bara Mhe. Benson Kigaila,

Kwengineko Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema aliachiliwa pia kwa dhamana katika kituo cha Polisi cha Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Lema anadai kuwa yeye alikamatwa hata kabla ya maandamano kuanza kwani alishushwa kutoka ndege mara tu ilipotua.

''Walinikamata nikiwa nashuka ndege, wanadai kosa langu ni kuanza maandamano nikiwa ndani ya ndege.'' alisema Lema.

Polisi hawakutoa maelezo zaidi baada ya kuachiliwa kwa viongozi hao.

TRT Afrika