Vikosi vya usalama vya Uturuki 'vimewakata makali' magaidi 942 tangu Januari 1 / Picha: AA 

Uturuki "imewakata makali " jumla ya magaidi 942 wa PKK/YPG tangu Januari 1, wakiwemo wale waliojificha kwa kuvuka mipaka ya Iraq na kaskazini mwa Syria, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ilisema Alhamisi.

"Magaidi 50 wamekatwa makali katika wiki iliyopita, ikiwa ni pamoja na Iraq na kaskazini mwa Syria, kwa mkakati wa kutokomesha ugaidi katika chanzo chake, ambayo tunatekeleza kwa uthabiti," afisa wa Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa nyuma katika mji mkuu Ankara.

Aliongeza kuwa jumla ya magaidi waliokatwa makali katika mwaka huu sasa imefikia 942.

Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kukata makali" kumaanisha kwamba magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kutekwa.

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha na kuvuka mpaka ili kupanga mashambulizi ya kigaidi. PKK/YPG - tawi la kundi la Syria - limetaka kuanzisha "ukanda wa kigaidi" katika maeneo ya mpaka wa Syria, karibu na Uturuki.

Operesheni ya mipaka

Uturuki imeanzisha operesheni kadhaa katika mpaka, kaskazini mwa Syria, kuzuia mipango ya kundi hilo la kigaidi.

Afisa huyo wa wizara hiyo alisema kuwa bohari moja kubwa zaidi ya risasi za kundi la kigaidi la PKK ilinaswa katika eneo la Operesheni Claw-Lock kaskazini mwa Iraq wiki hii, na jumla ya vipande 15,400 vya risasi za kukinga ndege vilitwaliwa.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na umoja wa ulaya - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, watoto na watoto wachanga.

YPG ni kitengo chake cha Syria.

Makundi ya kigaidi yanaendelea kushambulia raia na vitengo vya kijeshi kutoka mikoa mingine, haswa kaskazini mwa Syria, afisa huyo alisema.

"Kufikia Januari 1, jumla ya matukio 83 ya unyanyasaji na mashambulizi yalitekelezwa na kundi la kigaidi (PKK/YPG) katika maeneo ya operesheni zetu, na idadi ya magaidi waliopoteza maisha ilifika 699," aliongeza.

Kusimamisha kuvuka mipaka kinyume cha sheria

Kuhusu kuvuka mipaka kwa njia haramu kuingia Uturuki, alisema kutokana na hatua za ziada zenye ufanisi, mwaka huu watu 4,468, wakiwemo magaidi 347, ambao walijaribu kuvuka mipaka ya Uturuki, kinyume cha sheria walikamatwa tangu Januari tarehe mosi.

Karibu 132,000 walizuiliwa kabla ya kuvuka mpaka.

Uturuki imekuwa kituo muhimu cha kupitisha wahamiaji wasio wa kawaida ambao wanataka kuvuka kuingia Ulaya kuanza maisha mapya, haswa wale wanaokimbia vita na mateso.

Nchi hii, ambayo tayari inawahifadhi wakimbizi milioni nne, zaidi ya nchi nyingine yoyote duniani, inachukua hatua mpya katika mipaka yake kuzuia wimbi jipya la wahamiaji.

Makombora ya risasi yalipatikana pwani ya Bahari Nyeusi

Kuhusu mlipuko unaodhibitiwa wa makombora 28 yaliyopatikana kwenye ufuo wa Bahari Nyeusi huko Istanbul, afisa huyo alisema shughuli za uchunguzi chini ya maji zilifanywa katika eneo la mita za mraba 4,200.

"Jumla ya makombora 28 ya mizinga, ambayo yanachukuliwa kuwa ya vita vya Kidunia vya pili, yalitambuliwa. Risasi 11 kati ya zinazohusika, ambazo zinaweza kuondolewa, zililetwa kwa Kamandi ya Kikosi cha Ulinzi cha Chini ya Maji cha Uturuki (SAS), na 17 kati yao ziliharibiwa hapo hapo jana kwa njia iliyodhibitiwa," aliongeza.

Vyanzo vya Wizara ya Ulinzi ya Taifa, ambavyo viliomba kutotajwa majina kutokana na vikwazo vya kuzungumza na vyombo vya habari, vilisema hakuna tishio katika eneo hilo.

TRT Afrika