Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres amesema kila mtalii anaweza kuwa balozi wa amani/ Picha: Msemaji wa UN 

" Utalii huwaleta watu pamoja," hiyo ndio kauli kutoka kinywani kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Utalii.

" Katika Siku hii ya Utalii Duniani, tunatafakari juu ya uhusiano wa kina kati ya utalii na amani. Utalii endelevu unaweza kubadilisha jamii - kutengeneza ajira, kukuza ushirikishwaji na kuimarisha uchumi wa ndani," Guterres ameongeza.

Hata hivyo, ukosefu wa amani katika sehemu mbalimbali dunia kumedhoofisha sekta hiyo muhimu kwenye uchumi wa nchi. Mfano mzuri ni Sudan, ambapo vita kati ya jeshi la serikali na kikundi cha Rapid Response Forces (RSF), vilivyodumu kuanzia Aprili 2023, vimeathiri sekta hiyo muhimu.

Hii inafuatia mizozo ya ndani, iliyojitokeza toka kuondolewa kwa nguvu madarakani kwa Rais Omar el Bashir, mwaka 2019.

Sudan inafahamika zaidi kwa utajiri wake wa mapiramidi, ambayo idadi yake imeipita ile inayopatikana nchini Misri.

Takwimu zinaonesha kuwa, sekta za utalii na uchukuzi zilichangia asilimia 2.4 tu ya pato la taifa la Sudan, hadi kufikia mwaka 2019. Ukilinganisha na nchi nyingine barani Afrika, Sudan haina bahati ya kutembelewa na watalii wengi, huku migogoro isiyokwisha ikiwa imeathiri sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa.

Nchi zingine ambazo utalii wake umeathirika kutokana na vita, ni pamoja na Sudan Kusini, Ethiopia, Sahel pamoja na Mali.

" Kila msafiri anaweza kuwa balozi, akishirikiana kwa heshima na wakazi wa eneo hilo, akitambua utofauti wetu na ubinadamu wa pamoja, na maadili ambayo yanatuunganisha sisi sote," amesema Gutteres.

" Kwa kuthamini na kuhifadhi urithi wa kitamaduni na asili, inaweza kusaidia kupunguza mivutano na kukuza kuishi pamoja kwa amani. Utalii pia unaweza kukuza kutegemeana kwa uchumi kati ya majirani, kuhimiza ushirikiano na maendeleo ya amani," ameongeza Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.

Gutteres

TRT Afrika