Baraza la Usalama limeongeza vikwazo dhidi ya Sudan - ikiwa ni pamoja na kufungia mali, kuweka marufuku ya kusafiri na vikwazo vya silaha hadi Septemba 12, 2025.
Baraza hilo lenye nchi wanachama 15 liliamua kupitisha hatua hizo kwa mwaka mwingine, na uamuzi wa kuongeza muda huu utafanywa kabla ya tarehe Septemba 12, 2025.
Azimio nambari 1591 la Umoja wa Mataifa lilipitishwa awali na Baraza mwezi Machi 29, 2005, ili kuiwekea Sudan vikwazo kwa kulenga watu binafsi na vyombo vinavyohusika katika mzozo wa Darfur.
Pendekezo la kuongezwa muda wa vikwazo liliwakilishwa na Marekani.
"Uamuzi huu unatoa ishara muhimu kwao kwamba Jumuiya ya Kimataifa inasalia kuzingatia masaibu yao na imejitolea kuendeleza amani na usalama nchini Sudan na kanda," mwakilishi wa Marekani alisema katika kikao hicho.
Tangu kuanza kwa vita nchini Sudan Aprili 2023 kati ya Jeshi la Sudan na kikundi cha Rapid Support Forces, hali imezidi kuwa tata katika eneo la Darfur.
Mwakilishi huyo wa Sudan alielezea kwamba mashambulizi yanayoendelea dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia huko Darfur, ikiwa ni pamoja na vituo vya matibabu, yanayotekelezwa na kikundi cha Rapid Support Forces kwa kutumia mizinga nzito na silaha zilizopigwa marufuku kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Mwakilishi wa China alisema kuwa nchi yake inaunga mkono kuongezwa kwa muda wa vikwazo ili kusaidia "kuzuia mtiririko thabiti wa silaha haramu kwenye maeneoa ya vita" na kupunguza hali hiyo. Alisisitiza kuwa nchi wanachama wa UN watazingatia vikwazo vya silaha huku zikiheshimu kuwa Sudan ni nchi huru na ina mamlaka yake.
Sudan imesisitiza haja ya shinikizo la kimataifa kwa kikundi cha RSF kuwalipa fidia wananchi wa Sudan kutokana na hasara waliyoipata kupitia uporaji mkubwa na uharibifu mkubwa, ikisema hii ni sawa na RSF kuwa wagaidi.