Rais Ali Bongo inaripotiwa ameshikiliwa na wanajeshi katika makazi yake 

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, amesema anafuatilia kwa makini hali katika Jamhuri ya Gabon na kulaani vikali jaribio la mapinduzi nchini humo.

Amesema mapinduzi ya serikali sio njia ya kutatua mgogoro wake wa sasa wa baada ya uchaguzi.

Faki amesema mapinduzi ni ukiukaji wa katiba ya umoja wa Afrika ambayo inaunga mkono uchaguzi kama njia ya kubadilisha serikali.

Mwenyekiti huyu ameiomba jeshi nchini Gabon kuhakikisha kuwa rais Bongo na familia yake wako salama.

Tume hiyo ya kibara imehimiza wahusika wote wa kisiasa, kiraia na kijeshi nchini Gabonkutumau njia za amani, na kurejea kwa haraka kwa utaratibu wa kidemokrasia wa kikatiba nchini humo.

TRT Afrika