KIongozi wa kijeshi wa Chad Mahamat Déby alitangazwa mshindi rasmi wa uchaguzi wa Rais, Mei 6, 2024./ Picha Wengine 

Mweyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amekataa kuzungumza kuhusu ushindi wa kiongozi wa Chad, aliyeshinda uchguzi wa Urais.

Kiongozi wa kijeshi nchini humo, Mahamat Déby alitangazwa kama mshindi rasmi wa uchaguzi wa Rais, uliofanyika Mei 6, 2024 na hivyo kuendelea kubaki katika nyadhifa hiyo.

" Baraza la Amani na Usalama la AU ambalo ndio chombo pekee cha bara linalohusika na masuala ya amani na usalama kilipiga marufuku wanajeshi kugombea katika uchaguzi mara tu baraza la uongozi wa mpito wa jeshi lilishikilia uongozi nchini Chad," Ebba Kalondo, msemaji wa mwenyekiti wa tume ya Au ameeleza katika taarifa.

Katika mkutano wake wa Mei 11, 2023 baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lilizingatia kuongezwa kwa kipindi cha mpito nchini Chad na uongozi wa kijeshi kwa miezi 24 ikikataa kuongezwa kwa muda.

Wakati huo huo, mkutano huo uliweka msisitizo kwenye taarifa yake ya Mei 14, 2021 ambapo ilitoa wito kwa wanachama wa serikali hiyo ya mpito kutoshiriki katika uchaguzi.

" Kwa kufahamu kifungu hiki mamlaka ya mpito haikutaka AU iangalie uchaguzi hizi," Kalondo anaongeza.

Jenerali Déby alishiriki kwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na kushinda kwa asilimia 61.3 ya kura, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, huku mpinzani wake wa karibu, Waziri Mkuu Succes Masra, akishinda kwa asilimia 18.53.

" Kwa kuzingatia ukweli huu uliothibitishwa haiwezekani kwa mwenyekiti wa tume kutamka kuhusu matokeo ya uchaguzi kama huo isipokuwa kama atakiuka maamuzi ya Baraza la Umoja wa Afrika la amani na usalama, ambayo analazimika kuheshimu. Kwa hiyo ni juu ya baraza la amani na usalama kuamua hatima ya maamuzi yake," Kalondo amesema.

Baada ya kifo cha baba yake Idriss Déby, Mahamat Idriss Deby Itno, aliteuliwa kama kiongozi wa mpito, kwa kipindi cha miaka miwili hadi hapo utakapofanyika uchagzu mwingine.

Baba yake alifariki mwaka wa 2021 wakati wa vita na waasi alipokuwa amewatembelea wanajeshi wake.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT Afrika