Uingereza ina mpango wa kuwatuma wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda, jambo ambalo limezua utata / Picha:Wengine

Sheria ya Uingereza kuhusu mpango wake wenye utata wa kuwatuma wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda, inapuuza kanuni za haki za kimsingi, Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alisema Jumatatu.

"Madhara ya pamoja ya mswada huu, kujaribu kukinga hatua ya serikali dhidi ya uchunguzi wa kawaida wa kisheria, inapunguza moja kwa moja kanuni za msingi za haki za binadamu," Volker Turk alisema katika taarifa.

Serikali ya Uingereza imekuwa ikijaribu kusukuma sera ya uhamiaji ambayo inaweza kuruhusu kuhamishwa kwa makumi ya maelfu ya wanao omba hifadhi nchini Rwanda licha ya uamuzi wa Mahakama uliosema mpango huo ni kinyume cha sheria.

Lakini Waziri Mkuu Rishi Sunak anasema utawala wake unataka kupunguza idadi ya wahamiaji wasio wa kawaida wanaowasili nchini.

''Hakuna njia ya kuwazuia watu kuja hapa isipokuwa kama una kizuizi ambacho kinamaanisha kuwa watatumwa mahali pengine. Ni rahisi kama hivyo,'' Bw Sunak alisema wakati wa kuwasilisha kwa wabunge mwezi Desemba.

''Hiki ndicho kizuwizi chetu na tunafanya kila tuwezalo kuipata kwenye vitabu vya sheria na kuianzisha,” aliapa.

TRT Afrika