Bunge la Uganda limeitaka serikali kutafuta fidia kutoka kwa serikali ya Kenya kufuatia kuchomwa kwa Jumba la Uganda jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha tarehe 25 Juni 2024.
"Kamati ilipendekeza kwamba Serikali ya Uganda inapaswa kufuata fidia kutoka kwa serikali ya Kenya kwa uharibifu wa Jumba la Uganda House jijini Nairobi wakati wa ghasia za muswada wa fedha jijini humo ," alisema Achia Remigio mbunge wa Kaunti ya Pian, alipokuwa akiwasilisha ripoti ya Waraka wa Mfumo wa Bajeti wa 2025/26.
Katika mapendekezo ya bajeti ya FY2025/26, ubalozi wa Uganda huko Nairobi imetengewa zaidi ya dola milioni 1.1 (Sh 4.401Bn) kwa ajili ya kukarabati jengo hilo ingawa hii inaacha Ubalozi na pengo la ufadhili la zaid ya dola laki 258 (Shs949Mn) .
Bunge liliarifiwa kuwa Uganda House jijini Nairobi ilifanyiwa ukarabati kwa gharama ya jumla ya zadi ya dola milioni 7ambapo zadi ya dola milioni 6.6 ilikuwa kwa ajili ya kazi za mradi na zaidi ya laki 489 kwa ajili ya usimamizi wa ushauri.
Ukarabati huo ulikusudiwa kuongeza makusanyo ya kukodisha ya vyumba katika jumba hilo Uganda hadi zaidi ya dola milioni 1.08.
Tathmini ya kazi zaidi zilizopendekezwa ilikadiriwa kugharimu zaidi ya dola milioni 1.9 (UGX7.2Bn).