Serikali ya Uganda imependekeza mabadiliko katika ushuru ya nchi. Wizara hiyo imeweka mapendekezo yake katika Muswada wa Marekebisho ya Ushuru wa Bidhaa wa 2024 ambao uliwasilishwa Bungeni na Wizara ya Fedha.
Serikali imependekeza kutoza ushuru wa 5% kwa faida iliyopatikana kutokana na mauzo ya ardhi katika miji na manispaa, uuzaji wa mali ya kukodisha na uuzaji wa hisa katika kampuni binafsi.
Mlipakodi anatakiwa kulipa pesa hizi kwa Mamlaka ya kutoza Ushuru ya URA ndani ya siku 15 baada ya kuondoa mali au kulipa faini ikiwa ushuru haujatolewa ndani ya muda uliowekwa.
Bei ya ujenzi itaongezeka sasa huku kukiwa na pendekezo kutoka kwa wizara ya fedha kutoza ushuru wa dola 0.13 (Shilingi 500) kwa kila kilo 50 za saruji, vibandiko, mchanga, saruji nyeupe au chokaa,
Katika hatua ambayo huenda ikaongeza bei ya bidhaa hizo sokoni. Serikali pia imependekeza kutoza asilimia 10 au Shs75 kwa lita, chochote kilicho juu, kwenye maji ya madini, maji ya chupa na maji mengine kwa makusudi kwa ajili ya kunywa.
Serikali pia imependekeza kutoza ushuru kwa bidhaa za mafuta kama vile; petroli kwa dola 0.40 ( shilingi 1550) kwa lita moja.
Kwa mafuta ya gesi (gari, taa, kahawia ya injini) imependekeza pia ongezeko ya dola 0.32 ( Shilingi1230) kwa lita kwa mafuta ya taa pia iwe dola 0.13 ( Shilingi 500).
Wizara ya Fedha pia imependekeza kuondoa malipo ya ushuru kwa magari ya umeme yanayotengenezwa nchini Uganda, vifaa vya kuchaji vya magari ya umeme vilivyokusanywa nchini Uganda.
Pia inapendekeza malipo ya ushuru ya VAT kwenye bidhaa kama vile; majembe, dawa, mbolea na miche, majiko ya kupikia yanayotumia ethanol. Msamaha huo unapendekezwa kuendelea hadi tarehe 30 Juni 2028.