Timu ya waangalizia wa uchaguzi ipo Zimbabwe tayari kwa uchaguzi mkuu nchini humo / Picha kutoka AU

Waziri mkuu wa Uganda Ruhakana Rugunda ameteuliwa na Umoja wa Afrika, AU, kuongoza timu ya waangalizi katika uchaguzi mkuu wa Zimbabwe.

Rugudana anaongoza timu ya AU na jumiya ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

Watu milioni sita na laki tano nchini Zimbabwe wamejisajili kupiga kura kuchagua rais wa nchi hiyo tarehe 23 Agosti.

Emmerson Mnangagwa anawania muhula wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kama rais /Picha : Reuters 

Katika majimbo 10 ya nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika, wapiga kura pia watapiga kura kwa wawakilishi wa serikali za mitaa na wawakilishi wa bunge.

"Nimefurahi kujiunga na rais Goodluck Johnathan (Rais wa zamani wa Nigeria), katika kuongoza ujumbe wa waangalizi katika uchaguzi mkuu wa Agosti 23 nchini Zimbabwe," Rugunada amesema katika mtandao wa X.

"Tunawatakia watu wa Zimbabwe uchaguzi wa amani na wa kuaminika unaoakisi matakwa ya wananchi," ameongezea.

Timu ya waangalizi inajumuisha waangalizi 86 ambao ni pamoja na mabalozi walioidhinishwa na AU, maafisa wa bodi za usimamizi wa uchaguzi, wanachama wa mashirika ya kiraia barani Afrika.

Pia kuna wataalamu wa uchaguzi wa Afrika, wataalamu wa haki za binadamu, wataalamu wa jinsia na vyombo vya habari, na wawakilishi wa mashirika ya vijana.

Waangalizi hao wametoka nchi 23 ambazo ni pamoja na Kenya, Rwanda, Ushelisheli na Tanzania.

Waangalizi watatumwa kwa majimbo yote 16 ya uchaguzi nchini Zimbabwe.

Nelson Chamisa ni mgombeaji mkuu wa uchaguzi nchini Zimbabwe / Picha: Reuters 

Wagombea Zimbabwe

Jumla ya wagombea 11 wanakiangalia kiti cha urais.

Lakini wagombea wakuu katika kinyanganyiro cha kiti cha urais ni rais wa sasa Emmerson Mnangagwa. Emmerson mwenye umri ya miaka 80, anawania muhula wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kama rais.

Mgombea mwingine mkuu ni Nelson Chamisa akiwa na umri wa miaka 45. Yeye ni kiongozi wa upinzani.

TRT Afrika