Uganda ina huduma ya dharura isiyoweza kufikiwa kwa urahisi na yenye ubora duni. Wizara ya Afya Uganda imetoa masharti ya mpango wa kitaifa wa huduma za dharura.
Serikali ya Uganda imetambua hili na kuiweka kama kipaumbele. Ina nia ya kupanua utoaji wa huduma, mafunzo, ufuatiliaji, na tathmini ya utoaji wa huduma za dharura nchini.
"Sera hii ya Kitaifa ya Huduma za Matibabu ya Dharura inakuja katika kukabiliana na kilio cha umma juu ya mwitikio duni kwa dharura kutoka kwa eneo la dharura katika maeneo ya ajali, vituo vya afya visivyofanya kazi, huduma za ambulensi na ukosefu wa uratibu wa wadau mbalimbali," Wizara ya Afya inasema.
"Katika miezi sita iliyopita mmoja kati ya makazi 8 wameripoti kupata mahitaji ya dharura ya afya, " ripoti ya shirika la Twaweza limesema.
Twaweza ni asasi ya kiraia inayofanya kazi Uganda, Kenya na Tanzania.
Utafiti wao unaonyesha kuwa wananchi wengi Uganda huenda wakiwa na shida dharura ya kiafya watakimbilia majirani au watu walio karibu nao au hata kujaribu kufikia kituo cha afya karibu nao hii ni kwa sababu hawajui njia nyingine ya kuita msaada,
"Ni mtu mmoja tu kati ya 20 ambao hata wanajua kuwa kuna nambari ya kupiga kuomba msaada ya kiafya , ambayo haihitaji kulipiwa," ripoti ya Twaweza inaonesha.
Utafiti pia umeonesha kuwa hata watu wakijifikisha katika vituo vya afya , kupata huduma kunachelewa sana, Wengine waliohojiwa walisema mgonjwa anaweza kulazimika kungoja kwa zaidi ya dakika arobaini kabla ya kupata huduma,
Huduma ya dharura ya afya inaathiriwa zaidi kwasababu kuna upungufu wa vifaa vya matibabu na hata wahudumu wa kiafya.