Shirika la WFP linaonya kuwa rasilimali ya kusaidia mamilioni ya walioathiriwa DRC inapungua / Picha kutoka akaunti ya WFP Twitter (X)

Umoja wa mataifa unasema takriban watu milioni 6.3 ni wamelazimika kuhama makwao ndani ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Kati ya hayo, takriban milioni 6 wako ndani ya majimbo matatu ya mashariki mwa nchi hiyo.

Mizozo inaendelea katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini, na Ituri Mashariki mwa DRC kati ya serikali na vikundi vyenye silaha.

Pamoja na changamoto ya chakula, idadi ya watu, haswa wanawake, wasichana, na wavulana, wanakabiliwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Shirika la Chakula Duniani, WFP, linasema mzozo wa mashariki mwa DRC unaathiri uhaba wa chakula, utapiamlo, afya, elimu, upatikanaji wa maji safi na makazi.

"Utapiamlo unaathiri watu milioni 4.4, wakati ukosefu wa huduma muhimu umeongezeka zaidi ulinzi wa raia na kuchochea unyayasaji wa kijinsia" imesema katika taarifa.

Changamoto sasa ni kuwa rasilimali ya kuwahudumia mamilioni waliaothiriwa inazidi kupunguka.

"Ufadhili umekaribia kukauka; Mahitaji ya uendeshaji ya WFP yako hatarini. WFP imepokea ufadhili mdogo," Peter Musoko, Mkurugenzi wa WFP nchini DRC amesema.

"Hasa, mwezi Julai, WFP ilitoa msaada kwa baadhi ya watu milioni 1.2. Hata hivyo, bila ufadhili wa ziada, kuna uwezekano kwamba watu wengi zaidi wanaweza kuhatarisha kutopokea kwamba tutakaribia nusu ya lengo letu lililokusudiwa."

Ufadhili unawezesha WFP kununua mahitaji kama kunde, mafuta na chumvi, na hivyo kuhakikisha mbinu kamili ya lishe.

"WFP inahitaji dola za Marekani milioni 728 kwa juhudi zake za kukabiliana na kanda ya mashariki. Kwa kusikitisha, tunakabiliwa na pengo kubwa la ufadhili la Dola za Marekani milioni 567, sawa na asilimia 78 ya fedha zinazohitajika kwa muda wa miezi sita ijayo," Musoko ameongezea,

TRT Afrika