Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenya linaloungwa mkono na serikali siku ya Ijumaa lilisema maafisa wa serikali walipuuza "ripoti za kuaminika" ambazo zingeweza kuzuia vifo vya zaidi ya watu 400 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa madhehebu ya siku ya maangamizi.
Mabaki ya binadamu yaligunduliwa mwezi Aprili mwaka jana katika msitu wa Shakahola, eneo kubwa la misitu ambalo liko katika mji wa Bahari ya Hindi wa Malindi.
Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR), chombo kinachofadhiliwa na serikali, iliwakosoa maafisa wa usalama huko Malindi kwa "kupuuza wajibu na uzembe mkubwa."
"Hawakushindwa tu kuwa makini katika kukusanya na kuchukua hatua za kijasusi ili kuzuia mauaji ya Shakahola lakini pia walishindwa bila sababu yoyote kuchukua hatua kulingana na ripoti za kuaminika," Mwenyekiti wa KNCHR Roseline Odede alisema.
Kesi mahakamani
Aliyejiita kasisi Paul Nthenge Mackenzie anadaiwa kuwachochea wafuasi wake kufa njaa ili "kukutana na Yesu."
Wakati njaa inaonekana kuwa sababu kuu ya vifo, baadhi ya waathiriwa, ikiwa ni pamoja na watoto - walinyongwa, kupigwa au kuzidiwa, kulingana na uchunguzi wa maiti zilizofanywa na serikali.
Kati ya Aprili na Oktoba mwaka jana, jumla ya miili 429 ilitolewa kutoka kwenye makaburi yenye kina kirefu, huku watu wazima 67 na watoto 25 wakiokolewa, kulingana na rekodi za serikali.
KNCHR ilisema msimamo mkali wa Mackenzie, dereva wa zamani wa teksi, ulijitokeza katika kikao cha kamati ya mahakama mnamo Novemba 2019 lakini ulipuuzwa.
Mfuasi wa zamani wa Mackenzie alijaribu "kukata tamaa" na kusema yaliyokuwa yanajiri lakini pia alipuuzwa.
"Badala ya kuchunguza ukweli wa masuala yaliyoibuliwa, bibi huyo aliingiwa na woga baada ya kushutumiwa kwa kutoa shutuma zisizo na msingi," Odede alisema.
"Tume inasikitika kwamba hakuna vikwazo vinavyojulikana vilivyochukuliwa dhidi ya maafisa hao waliopuuza jukumu lao la kulinda mamia ya watu wakiwemo watoto ambao ama wamepotea, wamefariki au walijeruhiwa sana," KNCHR ilisema.
Mackenzie amekuwa kizuizini tangu mwezi Aprili huku uchunguzi ukikamilika.
Tangu wakati huo amefunguliwa mashtaka ya mauaji, kuua bila kukusudia, ugaidi na unyanyasaji wa watoto.