| Swahili
AFRIKA
2 DK KUSOMA
Tanzania yasema haina maambukizi ya Mpox
Hata hivyo,  Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia kwa karibu ugonjwa wa Mpox na kuchukua hatua stahiki kuzuia ugonjwa huu kuingia nchini humo.
Tanzania yasema haina maambukizi ya Mpox
Mtaalamu wa afya akimchunguza mtoto aliyeathirika na ugonjwa wa Mpox nchini DRC./Picha: Reuters / Others

Serikali ya Tanzania imesema kuwa hakuna maambukizi ya ugonjwa wa Mpox nchini humo.

Hata hivyo, Mganga Mkuu nchini humo Profesa Tumaini Nagu amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kufuatilia kwa karibu ugonjwa wa Mpox na kuchukua hatua stahiki kuzuia ugonjwa huu kuingia nchini humo.

"Mpaka sasa, hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitika kuwa na maambukizi ya Mpox na nchi yetu ni salama. Hata hivyo, tunahitaji kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na ugonjwa huu," ilisomeka taarifa ya Profesa Nagu, kama ilivyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Wizara ya Afya ya Tanzania.

Katika taarifa yake, Mganga Mkuu katika serikali ya Tanzania ameuasa umma kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huo kama vile kuepuka kugusana, kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kumbusu mtu mwenye dalili za Mpox, kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono mara kwa mara na kuepuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.

Pia imewataka watu kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Mpox na kama ikibidi, kuwahi katika vituo vya huduma za afya wanapoona dalili za ugonjwa wa Mpox.

"Vile vile, tumeimarisha vituo vya huduma, maabara na upatikanaji wa dawa, vifaa kinga na tiba ili kutoa huduma stahiki endapo utaingia nchini," amesema.

Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Mpox umeendelea kutolewa taarifa kutoka nchi mbalimbali duniani, ambapo hadi kufikia Juni 2024, jumla ya wagonjwa 99, 176 na vifo 208 vimethibitishwa.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Soma zaidi
Rais Samia wa Tanzania kuzindua mji wa serikali jijini Dodoma
Tanzania: Tume ya Jaji Lila yaanza kuchunguza waliopanga ghasia za Oktoba 29
Kiongozi wa Sudan Burhan kuhudhuria mkutano wa Urusi na Afrika jijini Moscow
Idadi ya walioambukizwa Ebola DRC yazidi 10,000, juhudi za kudhibiti ugonjwa huo zaendelea
Umoja wa Mataifa kuhitimisha misheni yake Somalia baada ya zaidi ya miaka 30
Mashambulizi ya droni ya RSF katika mitambo ya umeme yasababisha kukosekana kwa huduma Sudan
Chad na Ufaransa: Nani anamhitaji mwenzake zaidi?
Uganda kuweka karantini ya siku 21 kwa raia wanaorejea nchini kutoka DRC
Watu 22 wafariki nchini Kenya baada ya basi na lori kugongana kwenye barabara kuu
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, ametishia kuanza mgomo wa kula kuanzia 26 Oktoba
Wizara ya Afya nchini Kenya imeweka dawati la matibabu la saa 24 katika eneo la jengo lililoporomoka
Serikali yazindua uchunguzi wa pamoja kuhusu chanzo cha kuanguka kwa jengo jijini Nairobi
Kenya yathibitisha kifo cha pili kutokana na Ebola
Libya yakaribia kuungana tena, asema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Bunge la Kenya lapitisha mswada wa kuondolewa sharti la kutangaza matokeo ya uchaguzi mubashara
UN yaonya kuhusu hatari ya ukame katika nchi ya Sudan inayokabiliwa na vita
Ebola: Abiria wanaoingia Marekani kwa ndege wanatakiwa kueleza kama walisafiri DRC hivi karibuni
China yaonya kuhusu kuenea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati hadi Pembe ya Afrika
Polisi Afrika Kusini wachunguza kifo cha raia kigeni mjini Durban
Maambukizi ya Ebola yakaribia 10,000: WHO