Tanzania na Uturuki zatia saini mkataba sita. / Picha: AA

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi za Uturuki za kutatua mizozo ya kimataifa kwa amani.

"Pia tunaunga mkono wito wa dharura wa kusitisha mapigano kwa manufaa ya watu wa Gaza. Zaidi ya hayo, tunaunga mkono kuingizwa kwa misaada ya kibinadamu bila pingamizi yoyote ," Hassan alisema katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi kule Ikulu ya Rais wa Uturuki, alipokuwa akikutana na Rais Recep Tayyip Erdogan mjini Ankara.

Hassan alibainisha kuwa alikaribishwa kwa furaha mjini Uturuki na akaishukuru nchi hiyo.

Alisema Tanzania inasisitiza dhamira yake ya kuimarisha uhusiano wenye manufaa kati ya nchi hizo mbili.

"Uturuki kwa hakika ni mshirika wa thamani, na ziara yangu hapa inathibitisha jinsi tunavyothamini ushirikiano huu. Tulijadili vizuri sana maswala katika sekta mbalimbali wakati wa mkutano wetu wa pande mbili,"

Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania

Kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia

Hassan alisema kuwa Erdogan na yeye walijadili kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi, hasa katika sekta ya uzalishaji na kijamii.

Alisisitiza kuwa mahusiano yatachangia ukuaji wa uchumi wa nchi zote mbili.

"Nilitoa shukrani zangu kwa Uturuki katika suala la ushirikiano wa pande mbili. Niliwashukuru kwa msaada wao wa maendeleo na msaada wao kwa sekta ya elimu na afya katika nchi yetu. Niliwashukuru sana kwa msaada wao muhimu kwa miundombinu na ukuzaji wa rasilimali watu," alisema. alisema.

Viongozi wote wawili walitia saini mikataba sita ya maelewano, kwa mujibu wa rais wa Tanzania.

"Utaalamu na maarifa kutoka Uturuki yanahamishiwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na miradi yetu muhimu zaidi.

Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa reli ya SGR, na nilisisitiza kuunga mkono kwa Tanzania katika kufanikisha miradi hii, na kwa utekelezaji wake, tutapiga hatua kuelekea malengo yetu ya maendeleo. Mawaziri wetu, wataalam, watakutana ili kuunda mfumo wa ushirikiano katika maeneo yaliyokubaliwa, "alisema.

Ushirikiano katika biashara na uwekezaji

Hassan alielezea furaha yake kwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Tume ya Pamoja ya Uchumi ya Tanzania na Uturuki (JEC), na kusema kuwa Tanzania ina mpango wa kuwasiliana na sekta binafsi na watendaji wa Uturuki kuhusu ushirikiano katika biashara na uwekezaji.

Pia alibainisha kuwa Tanzania itafanya mkutano mjini Istanbul siku ya Ijumaa ukiangazia jumbe tatu kuu. "Mojawapo ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na wawekezaji na wafanyabiashara wa Uturuki katika nchi yetu. Pili, tutasisitiza uwekezaji ambao wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza kufanya, nafasi ya kimkakati ya soko wanayoweza kutoa, na fursa za kimkakati za soko ili kampuni za Uturuki zifanye biashara zaidi nasi," alisema.

Hassan alibainisha kuwa majadiliano yatafanyika kuhusu usafiri, "uchumi wa bluu", viwanda, kilimo na utalii.

Aliongeza kuwa Tanzania ilibadilishana mawazo na Erdogan kuhusu masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.

Hassan alimshukuru Erdogan kwa rambirambi zake kuhusiana na vifo vya watoto wanane nchini Tanzania kutokana na mvua kubwa.

Alisema kuwa mkutano wenye matunda mengi na Erdogan ulikamilika vizuri.

"Nina hakika kwamba kwa juhudi zetu za pamoja, Tanzania na Uturuki zitaendeleza ushirikiano wao wenye nguvu na ufanisi unaozingatia maadili ya pamoja," alisema hivyo huku akimkaribisha Erdogan nchini Tanzania.

TRT World