Katika muongo uliopita China imefadhili miradi ya miundombinu, kama vile reli, mitambo ya kuzalisha umeme na bandari,  kote barani Afrika/ Picha: Reuters 

Tanzania na Burundi zimetia saini makubaliano na makampuni mawili ya China kujenga reli kati ya nchi hizo mbili za Afrika kwa ajili ya kusafirisha madini ya vyuma metali, ikiwa ni pamoja na madini ya nikeli ya betri, hadi bandari ya jiji la Dar es Salaam.

Ubia huo wa $2.15 bilioni utajengwa na China Railway Engineering Group Ltd na China Railway Engineering Design and Consulting Group, Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Makame Mbarawa alisema wakati wa hafla ya kutiliana saini Jumatano.

''Mradi huu utafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),'' waziri wa fedha wa Tanzania Mwigulu Nchemba alisema.

Mataifa hayo mawili yanatarajia njia ya kupima kiwango cha kilomita 282 (maili 175) kusafirisha tani milioni tatu za madini kila mwaka, wizara ya fedha ya Tanzania ilisema mwaka jana.

Katika muongo uliopita China imefadhili miradi ya miundombinu, kama vile reli, mitambo ya kuzalisha umeme na bandari, na kote barani Afrika kupitia Mpango wake wa Ukanda na Barabara.

Reuters