Sudan imekataa Keny kuongoza timu ya nchi tano ambazo zimeteuliwa na IGAD kufanya upatanishi Sudan / Picha: Reuters

Sudan Jumatatu ilikataa mwaliko wa Kenya wa mkutano wa Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo (IGAD) kujadili mzozo wa Sudan.

Wiki iliyopita, IGAD ilitangaza kuunda kamati inayoongozwa na Kenya na Sudan Kusini kutafuta suluhu la mzozo wa Sudan. Ethiopia na Somalia ni wanachama wa kamati hiyo.

Katika taarifa yake, wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilisema haikubali mwaliko wa Kenya wa kufanya mkutano wa mawaziri wa IGAD, wa nchi zilizochaguliwa kufanya upatanishi Sudan.

"Sudan bado inasubiri jibu kutoka kwa mamalaka ya kikanda ya IGAD kuhusu pingamizi lake la uenyekiti wa Kenya kwa kundi la wapatanishi," ilisema taarifa hiyo.

Wizara hiyo haswa ilikataa maelezo ya Kenya kuhusu mzozo wa Sudan kama "mapambano kati ya majenerali wawili".

Sudan imeathiriwa na mapigano kati ya jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo wa Rapid Support Forces, RSF, tangu Aprili, katika mzozo ulioua karibu watu 1,000 na kujeruhi wengine 5,000, kulingana na madakitari nchini .

Kiini cha mgogoro unaoendelea ni watu wawili wanaopingana: mkuu wa jeshi la sudan Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti.

Tangu Oktoba 2021, waziri mkuu wakati jeshi lilipofuta serikali ya mpito ya Abdalla Hamdok na kutangaza hali ya hatari, Sudan imekuwa bila serikali inayofanya kazi.

Hatua hiyo ililaaniwa vikali na vikosi vya kisiasa kama "mapinduzi."

Kipindi cha mpito, kilichoanza Agosti 2019 kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir, kilipangwa kukamilika kwa uchaguzi mapema 2024.

TRT Afrika