Jeshi la Sudan Jumapili lilikaribisha kuhama kwa kamanda mkuu wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), Abuagla Keikal, pamoja na baadhi ya wanajeshi wake, kuashiria kile ilichosema kuwa ni mara ya kwanza kwa kiongozi mkuu kuondoka kwenye kundi hilo.
Duru zinaarifu kuwa Keikal alijisalimisha kwa jeshi siku ya Ijumaa nakupokewa na viongozi wa jeshi.
Msemaji wa jeshi la Sudan Mohamed Ibrahim alipongeza hatua ya Keikal na kikundi cha wapiganaji wake kama chaguo bora.
"Amechagua upande wa haki na taifa leo baada ya kuacha safu ya waasi na kuamua kupigana pamoja na vikosi vyetu." alisema Ibrahim.
Jeshi la taifa pia liliongeza kuwa Kakil na askari wake wengi walitambua "uongo na ubatili wa madai yaliyotolewa na wanamgambo wa kigaidi wa Al Dighlo na wasaidizi wao," ambao walikuwa "zana za bei nafuu" zilizotumiwa kuendeleza ajenda ya kimataifa na ya kikanda.
Video inayosambaa kwenye mitandao ya X inamuonyesha Kakil akitabasamu na kupiga picha na wanajeshi wa jeshi la Sudan huku wakaazi wa eneo hilo wakisherehekea.
Kufikia Jumapili, hakuna maelezo yaliyotolewa juu yamazingira yaliyopelekea kujisalimisha kwake wala iwapo kuna masharti yoyote.
Abuagla Keikal ilikuwa kamanda mkuu wa RSF katika jimbo la AL Jazira mashariki ya kati ya nchi linalozungukwa na mito za Blue Nile na White Nile.
Al Jazira inajulikana kama jimbo linalozalisha pamba kwa umwagiliaji kwani ni eneo lenye watu wengi ambalo linafaa kwa kilimo.
Kujisalimisha kwa Keikal kutoka eneo hilo kuna maana kuwa Jeshi la taifa linaweza kudhibiti jimbo hilo.
Bado hakuna jibu lolote kutoka kwa viongozi wakuu wa RSF kuhusu tangazo hilo.