#KTT97 : UN chief Guterres visits Somalia / Photo: AFP

Serikali ya Somalia inasema iko tayari kuchukua jukumu la usalama wa nchi wakati baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha mpito cha Umoja wa Afrika , yaani African Transition Misison in Somalia , wataondoka.

Wanajeshi 2000 wa kikosi cha ATMIS wanatarajiwa kuondoka nchini Somalia katika mpangilio wa kuipa Somali uwezo wa kuendesha ulinzi wa nchi.

" Vikosi vya jeshi la kitaifa la Somalia na vikosi vya Usalama vya Somalia viko tayari huku Somalia ikielekea kwenye sura inayofuata ya kumudu usalama wake nchini kote," taarifa kutoka wizara ya Ulinzi nchini Somalia imesema.

Burundi, Djibouti, Kenya, Ethiopia and Uganda zimechangia zaidi ya maofisa 20,000 katika Ujumbe wa Mpito wa Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS).

"Utawala wa Somalia katika kipindi cha miezi michache iliyopita uliunda vikosi kwa msaada kutoka nchi marafiki ambao watakuwa wakikabidhiwa majukumu ya wanajeshi 2000 wa ATMIS ambao wataondoka mwisho wa mwezi wa Juni 2023 kulingana na azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataifa, " taarifa hiyo imeongezea.

ATMIS inahusisha wanajeshi, polisi na raia, Iliidhinishwa na Umoja wa Afrika na kupewa mamlaka na mabaraza za usalama za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

ATMIS ilianza kufanya kazi tarehe 1 Aprili 2022 baada ya Umoja wa Afrika kuamua ichukue hatamu ya ujumbe wa Umoja wa Afrika chini Somalia AMISOM .

AMISOM ambayo illikuwa imeundwa 2007 na umoja wa Afrika ilikuwa na majukumu ya kusaidia Somalia kuimarisha uslama na kupigana na tishio la wanamgambo wa Al Shabaab.

Kwa mujibu wa azimio nambari 2670 la Umoja wa Mataifa, ATMIS inatarajiwa kupunguza wanajeshi 2000 mwishoni mwa mwezi huu na kukabidhi majukumu ya usalama kwa vikosi vya usalama vya Somalia.

Ujumbe wa Amani wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kuondoka kikamilifu Somalia ifikapo tarehe 31 Desemba 2024.

TRT Afrika
Tovuti hii hutumia vidakuzi. Kwa kuendelea kuangalia tovuti hii, unakubaliana na utumizi wa vidakuziSera ya Vidakuzi
Kubali