Shirika la Ndege la Uturuki kuongeza safari zake nchini Tanzani. / Picha: AA

Shirika hilo hivi sasa litatua mara 14 kwa wiki katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro-KIA, kutoka mara nne kwa wiki.

Ama kwa upande wa Zanzibar, Shirika hilo hivi sasa litakuwa na ratiba ya safari 14 kwa wiki, ambapo kila siku litakuwa na safari mbili.

Katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, Shirika la Ndege la Uturuki awali lilikuwa linatua mara 7, lakini kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika hilo, hivi sasa litakuwa linatua mara 10 kwa wiki.Ukuaji huu, utaiwezesha Tanzania kufikika kwa urahisi zaidi, huku ukiwapa wasafiri fursa zaidi ya kusafiri.

Tanzania inajulikana kwa utajiri wake wa mbuga za wanyama, Mlima Kilimanjaro pamoja na fukwe zake za kuvutia za Zanzibar.

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imekaribisha hatua hio, ikiangazia uwezo wake wa kukuza sekta ya utalii nchini na biashara za ndani.

TRT Afrika