Rais wa Tunisia Kais Saied alishinda tena uchaguzi kwa ushindi wa mkubwa katika matokeo yaliyotangazwa Jumatatu baada ya msimu wa kampeni ambao ulishuhudia wapinzani wake wakifungwa pamoja na waandishi wa habari, wanaharakati na mawakili.
Mamlaka Huru ya Juu ya Uchaguzi ya nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika, inayojulikana kama ISIE, ilisema Jumatatu jioni kwamba Saied ameshinda 90.7% ya kura - jambo linaloakisi jinsi wafuasi wake walivyoshiriki katika kinyang'anyiro cha Jumapili huku wengi wa wapinzani wake wakichagua kususia.
Mpinzani wake wa karibu, mfanyabiashara Ayachi Zammel, alishinda 7.4 ya kura baada ya kukaa gerezani kwa muda mwingi wa msimu wa kampeni akikabiliwa na uhalifu unaohusiana na uchaguzi.
Maafisa wa uchaguzi waliripoti asilimia 28.8 ya wapiga kura waliojitokeza - idadi ndogo sana kuliko duru ya kwanza ya uchaguzi uliopita nchini.
Ilikuwa ni kinyang'anyiro cha tatu cha urais nchini Tunisia tangu Mapinduzi ya Nchi Kiarabu ya 2011, wakati maandamano ya "mkate, uhuru na utu" yalisababisha kuondolewa kwa Rais Zine El Abidine Ben Ali.
Wapinzani wafungwa jela
Katika miaka iliyofuata, Tunisia iliweka katiba mpya na kuunda demokrasia ya vyama vingi. Walakini, Saied alianza kuvunja taasisi mpya za nchi miaka miwili baada ya kuchukua ofisi.
Mnamo Julai 2021, alitangaza hali ya hatari, akasimamisha bunge na kuandika upya katiba ili kudhibiti mamlaka mamlaka ya urais. Katika muhula wake wa kwanza madarakani, mamlaka ilianzisha wimbi la ukandamizaji kwa jumuiya ya kiraia iliyokuwa hai nchini humo.
Mnamo 2023, baadhi ya wapinzani wake mashuhuri kutoka katika wigo wa kisiasa walitupwa gerezani, akiwemo kiongozi wa mrengo wa kulia Abir Moussi na mrengo wa kiislamu Rached Ghannouchi, mwanzilishi mwenza wa chama cha Ennahda na spika wa zamani wa bunge la Tunisia.
Makumi ya wengine walifungwa gerezani kwa makosa ya kuchochea machafuko, kudhoofisha usalama wa serikali na kukiuka sheria tata ya kupinga habari ghushi ambayo wakosoaji wanasema imekuwa ikitumika kuzima upinzani.
Wagombea wengi walizuiliwa kushiriki
Kasi ya kukamatwa kwa watu hao iliongezeka mapema mwaka huu, wakati mamlaka ilipoanza kuwalenga wanasheria wa ziada, waandishi wa habari, wanaharakati wa uhamiaji na mkuu wa zamani wa Tume ya Ukweli na Utu baada ya Mapinduzi ya Nchi za Kiarabu.
Makumi ya wagombea walikuwa wameonyesha nia ya kuchuana na rais, na 17 waliwasilisha makaratasi ya awali ya kushiriki katika kinyang'anyiro cha Jumapili.
Hata hivyo, wajumbe wa tume ya uchaguzi waliidhinisha watatu pekee.
Baada ya kuchapishwa kwa orodha ya mwisho ya wagombea, Zammel alifungwa jela mara moja.
Jukumu la tume na wajumbe wake, ambao wote wameteuliwa na rais, lilianza kuchunguzwa wakati wa msimu wa kampeni. Walikaidi maamuzi ya mahakama iliyowaamuru kuwarejesha wawaniaji watatu ambao walikuwa wamewakataa hapo awali.
Baadaye bunge lilipitisha sheria ya kuondoa mamlaka kutoka kwa mahakama za utawala.