Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), ambayo inasimamia sekta ya michezo ya kiteknolojia imetoa sera mpya ya kamari nchini humo / Picha: AP

Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), ambayo inasimamia sekta ya michezo ya kiteknolojia imetoa sera mpya ya uendeshaji wa kamari nchini humo.

Sera hiyo inalenga zaidi kudhibiti sekta ndogo ya kamari na kupata manufaa ya kiuchumi huku ikipunguza madhara ya kiuchumi na kiafya kwa wachezaji.

Kati ya 2013 na 2019, sekta ya kamari nchini Rwanda imeingiza mapato ya jumla ya zaidi ya dola 193,000,000 ( Rwf264.3 bilioni) na ushuru wa zaidi ya dola milioni 6.4 (Rwf8.8 bilioni ).

Michango kwa Bodi ya Hifadhi ya Jamii ya Rwanda (RSSB) ilifikia zaidi ya dola 455,320 ( Rwf623.2 milioni) wakati ushuru na ada ulifikia zaidi ya dola 244,172 (Rwf334.2 milioni).

Serikali imesema Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) itatoa leseni upya kwa waendeshaji wote wa kamari, waliopo na wapya.

Inasema mchakato huu utakuwa na uwazi na utatumia vigezo vya tathmini vinavyofanana ili kuhakikisha utiifu wa viwango vya juu vya uwajibikaji kwa jamii, uwazi wa kifedha na usawa wa soko.

Chini ya sheria mpya waendeshaji wa biashara ya kamari nchini Rwanda watakabiliwa na mahitaji ya leseni chini ya sera mpya, ikijumuisha majengo yanayoidhinishwa ili kukakikisha viwango vya usalama na mchango wa biashara kwa kiuchumi.

Sera mpya pia inalenga kuimarisha ulinzi wa watumiaji na uwajibikaji kwa jamii kwa hatua kwa mfano ni lazima wahusika kuweka ujumbe wa lazima katika matangazo kuhusu uthibitishaji wa umri na wateja kujitambulisha ili kuhakikisha kuwa kuna uwajibikaji kwa wanaohuska na kamari.

Pia inahitaji waendeshaji wa biashara hii kutoa programu za usaidizi kwa wale walioathiriwa na madhara yanayohusiana na kamari na kufanya kazi kwa karibu na huduma za afya na kijamii.

TRT Afrika