Brigedia Jenerali Patrick Kauretwa aliteuliwa kuwa Rais wa Mahakama Kuu ya Kijeshi/ Picha: Rwanda Defence Forces

Rwanda imeapisha maafisa wapya wa kijeshi wa Mahakama ya Kijeshi.

Dkt. Edouard Ngirente, Makamu wa Rais wa Rwanda aliongoza Sherehe hiyo.

Kufuatia kibali cha Baraza la Mawaziri cha Novemba 9, 2024, Brigedia Jenerali Patrick Kauretwa aliteuliwa kuwa Rais wa Mahakama Kuu ya Kijeshi.

Lt. Darcy Ndayishimiye na Lt. Thérèse Mukasakindi, na Majaji wawili katika Mahakama ya Kijeshi, Kapteni Moses Ndoba na Lt. Victor Kamanda.

Waziri Mkuu, Dkt. Edouard Ngirente aliwataka viongozi walioapishwa hivi karibuni kutanguliza maendeleo ya kitaaluma/ Picha: Rwanda Defence Forces.

Waziri Mkuu wa Rwanda Dkt. Ngirente aliwataka viongozi walioapishwa hivi karibuni kutanguliza maendeleo ya kitaaluma.

Aidha alisisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia katika kazi zao za kila siku ili kuongeza ufanisi, utendaji kazi na utoaji huduma.

Mfumo wa haki za kijeshi unajumuisha mahakama mbili za kijeshi yaani Mahakama Kuu ya Kijeshi, Mahakama ya Kijeshi; na Idara ya Mashtaka ya Kijeshi.

Mahakama za kijeshi zinajumuisha aina moja ya mahakama maalum zilizoanzishwa na Katiba ya Jamhuri ya Rwanda. Waamuzi lazima wawe wanajeshi.

Wizara ya Usalama ya Rwanda inasema Mahakama ya Kijeshi inahusika na Makosa ya jinai yanayoshukiwa kufanywa na wanajeshi. Madhumuni ya kimsingi inasema ni kudumisha utulivu na nidhamu kwa kuwawajibisha wahalifu wa kijeshi wakivunja sheria.

Kesi ya fidia inayotokana na kesi ya uhalifu iliyofanywa na afisa wa jeshi inaweza pia kuwasilishwa katika mahakama hiyo.

TRT Afrika