Rwanda imeboresha sheria yake ya miaka 27 ya ubinafsishaji   / Picha: Getty Images

Rwanda inasema kufanya mabadiliko kwa sheria yake ya ubinafsishaji kutaiwezesha kuongeza ufanisi, uwazi, na kuboresha tija katika kubinafsisha mali ya serikali.

Mabadiliko yapi yamefanywa katika sheria hii ambayo imekuwepo kwa miaka 27?

  • Sheria mpya imeruhusu kutengenezwa kwa kamati inayosimamia ubinafsishaji
  • Serikali inahifadhi haki ya kumiliki tena kampuni iliyobinafsishwa inayomilikiwa na serikali ikiwa mmiliki wa kampuni atashindwa kutimiza majukumu yaliyokubaliwa kama ilivyoainishwa chini ya makubaliano ya ubinafsishaji.
  • Sheria imeweka vipengele vya kuhakikisha kuwaubinafsishaji unafanyika kwa njia inayostahili, ili kuhusisha uwazi, haki na ushirikishwaji, ufanisi na uendelevu na thamani ya pesa.
  • Sheria mpya inaleta "hisa za dhahabu" ambazo ni mtaji wa kampuni iliyobinafsishwa ya Serikali na ambayo inabeba haki maalum kama ilivyowakilishwa kwenye vifungu vya ushirika wa kampuni hiyo na kuiwezesha serikali kulinda maslahi ya umma.

TRT Afrika