Serikali inasema masharti mapya yanalenga kuwapa wananchi ubora wa maisha / Picha: Getty Images

Rwanda imetoa uamuzi kuwa wakati wa usiku biashara zitafungwa saa saba alfajiri siku za jumatatu hadi Ijumaa na saa nane alfajiri siku za wikiendi.

"Uamuzi unalenga kuweka usawa katika vipaumbele vya Rwanda, ikiwa ni pamoja na kuifanya miji ya Rwanda kuwa mahali pazuri pa kuishi, lakini pia kuhakikisha kuwa Wanyarwanda wanakuwa na hali nzuri ya maisha ," Mkurugenzi mkuu wa Rwanda Development Board, Clare Akamanzi amefafanua.

Baraza la mawaziri limesema ni ni kudhibiti burudani ya usiku na uchafuzi wa kelele.

Uamuzi huu umezua utata huku biashara zikitegemea wateja wengi usiku zikidai kuwa mapato yao yatapungua.

Serikali sasa inasema itafanya uamuzi mwingine kuhusu biashara ambazo zitaruhusiwa kukiuka masharti hayo mapya.

"Kabla ya Septemba, Rwanda Development Board itatoa orodha ya biashara hizo. Kati ya biashara ambazo tunaona zinahitaji kupewa rushwa kuendela kufungua ni maduka aina ya 'supermarkets', maduka ya kuuza dawa," Akamanzi amesema.

Sekta za burudani pia zitazingatiwa.

" Wakati mwingine tutakuwa na tamasha ambazo ni lazima ziendeshwe baada ya wakati uliowekwa , pia kunaweza kuwa na vilabu ambavyo vinafungua baada ya wakati huo," Akamanzi ameongeza.

Biashara ambazo zitaruhusiwa kukaa wazi baada ya wakati uliowekwa na sheria zitapewa matarajio ya serikali ya kutimiza.

TRT Afrika