Raia wa Rwanda hawatahitaji tena visa ili kusafiri hadi Ushelisheli.
"Ushelisheli na Rwanda zina nia ya pamoja ya kuboresha hali ya maisha kwa raia wetu wote, kufanya kazi bega kwa bega na washirika katika kanda, na kwingineko." Kagame alisema Alhamisi.
Ushelisheli ni kati ya nchi za visiwa vidogo barani Afrika.
Nchi hiyo iliyo katika bahari ya hindi inategemea sana utalii. Kufikia Juni 2023, tayari imevutia watalii 160,959, na kupokea zaidi ya dola 360 kutoka kwa sekta hiyo mwaka huu.
"Kama Mwenyekiti wa Ofisi ya Jumuiya ya Madola, Rwanda imejitolea kusaidia nchi zinazoendelea za visiwa vidogo ambazo zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi," Kagame aliongezea.
Nchi hizo mbili zimekubali kuondoa vibali vya usafiri kati yao kwa ajili ya kuongeza utalii na biashara kati yao.
"Rwanda inachukuliwa kuwa mojawapo ya nchi zenye usalama ulimwenguni, wanawake wanajikuta katika hali ya usalama kamili na tunataka kuiga mfano wako," rais wa Ushelisheli Wavel Ramkalawan alisema.