Rwanda ilithibitisha maambukizi ya kwanza ya virusi vya Marburg mnamo Septemba 27, 2024 / Picha: Wengine 

Rwanda itatangaza rasmi mwisho wa mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Marburg mnamo Ijumaa, Disemba 20, 2024.

Marburg (MVD) ni homa hatari ya kuvuja damu isiyo na chanjo au tiba inayojulikana na imeuweka ulimwengu katika tahadhari ya afya ambapo wanasayansi walikuwa katika harakati ya kutafuta chanjo.

Mlipuko unaweza kuzingatiwa kuwa umeisha iwapo hakuna maambukizi mapya yatakayoripotiwa kwa siku 42 .

Kufikia Disemba 18, 2024 itakuwa imepita siku 47 bila maambukizi mapya na siku 41 tangu mgonjwa wa mwisho kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Wizara ya Afya haijaripoti kesi yoyote mpya tangu Oktoba 31.

Rwanda ilithibitisha kuwepo kwa maambukizi ya kwanza ya virusi vya Marburg mnamo Septemba 27.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali, wagonjwa 15 wamefariki kutokana na ugonjwa huo. Hakuna vifo vyengine vilivyorekodiwa tangu Oktoba 15.

TRT Afrika